Dec 24, 2012

MERRY X-MAS N HAPPY 2013

MILLARD AYO: LEO MIAKA 6 NYUMA

ALICHOANDIKA MILLARD AYO KATIKA PAGE YAKE YA FACEBOOK IMENIFANYA KUFIKIRIA V2 VINGI SANA.. Kama umemfuatilia huyu jamaa, ana bonge la History ingawa huwa analitoa nusu nusu kama hivi..

HIKI ndicho alichoandika..

"Miaka 6 iliyopita wiki kama hii ndio nilipata tuzo ya kwanza ya Utangazaji kutoka Tanzania Radio Awards, nikapandishwa mshahara toka elfu tano mpaka elfu kumi kwa wiki kwenye radio niliyokua nikifanyia kazi, sikutamani kufanya kazi nyingine japo nilikua naishi kwenye hali ngumu sana, niliahidi nitapambana ili nifanikiwe kwa hii kazi kwa sababu naamini Mungu ameweka kitu ndani yangu, nasema Amen leo nina maisha ninayoridhika nayo kabisa tena sana, Namshukuru Mungu sana kwa hilo! hii ni maalum kwa watu wangu wote wa nguvu ambao wanapitia shida, hawana kazi au wanafanya kazi lakini mafanikio hawayaoni, wanatafuta kazi kila siku hawapati, ukweli ni kwamba SUBIRA ni kila kitu, Nidhamu ni kila kitu, Maombi ni kila kitu, Kujituma ni kila kitu! kutokakuta tamaa ndio muhimu kabisa."
Millard akihojiana na Rozee..
Kila la kheri kaka ktk kazi zako..

Dec 23, 2012

Dec 22, 2012

SHILOLE&CHILLAH - DUDU Video

Official Video ya msanii SHILOLE feat. CHILLAH. Nyimbo inaitwa DUDU na audio imetengenezwa na C9 wa KIRI RECORDS. Video imefanywa na KWETU STUDIOS, Directed by Msafiri Shabani.

YOUR NEW MISS EAST AFRICA

Ni m'T'Zee Jocelyne Dyna Maro (22)
Walipokuwa Top 5.
Jocelyne Dyna Maro (22) Miss East Africa Tanzania ametangazwa mshindi katika shindano hilo lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam akiwashinda warembo wenzake kutoka mataifa mbalimbali ya Ukanda wa Afrika Mashariki na nchi Jirani na Ukanda huo. Jocelyne ni mchaga ameishi Uingereza, Afrika Kusini, Kenya na Ivory Coast.

Jocelyne Maro Mtanzania wa kwanza kushinda taji hilo toka lililpoanzishwa amejinyakulia zawadi zenye thmamani ya dola za kimarekani 30,000 likiwemo Gari aina ya Toyota Verossa, mara baada ya majaji kumtangaza mrembo huyo ukumbi mzima ulilipuka kwa shangwe huku watu mbalimbali wakimpongeza kwa ushindi wake.

DIS TYM 2NAUZA KWA CODE

Dec 21, 2012

OFA: EL-SHADDAI REKODI KWA NUSU GHARAMA

C.E.O George akiwa Maeneo ya Studio
C.E.O. wa El - Shaddai Record's, George David, waliopo Maghorofani kituo cha marolli karibu na kituo cha mafuta. Wametoa OFA maalumu ktk msimu huu wa X-Mas na Mwaka Mpya kwa kila Recording kwa nusu gharama.

Akiongea hilo katika mitandao yake binafsi na blog yao, amesema kuwa ametoa Ofa hiyo kwa ajili ya kila mtu  na ni kwa Nyimbo (audio), Matangazo na Jingles za aina zote kwa Nusu Gharama kama ilivokuwa kawaida.

Na huu ni moja kati ya ujumbe ulioandikwa na CEO huyo ktk FaceBook.. "NATOA OFFER KURECORD KWA NUSU GHARAMA KWA MEMBER YOYOTE WA EL SHADDAI RECORDZ AMBAYE ANAIMBA MUZIKI WA AINA YOYOTE KTK MSIMU HUU WA X - MASS NA MWAKA MPYA.KARIBUNI SANA"..

Mawasiliano yao ni 0752 513 276. Mnakaribishwa.

ANGALIA HII LIVE, BONGE LA KIPAJI


LORD EYEZ: UKWELI KUHUSU MIMI, RAY C, MADAWA&WIZI.

Baada ya kimya cha muda mrefu, msanii wa Hip Hop Tanzania kutoka ktk kundi la WEUSI, LORD EYEZ, amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu habari na kila kinachoendelea kuhusu yeye.

Lord Eyez amesema kuwa ameathirika sana kutokana na taarifa zilizokuwa zinaendelea kusambaa kuhusu yeye, lakini kwa watu waliomfahamu walijua kuwa ni janga tuu na wasiomjua ilikuwa kama vile ila habari hizo sio za kweli..

Kitu kilichotokea nilipigiwa simu nikasema nilipo mara zilitokea ndinga ghafra na kuatack kwangu wakiwa na Dimpoz. Walikuwa kama watu 15 na gari zao 15 wakidai vifaa vya Ommy vimeibiwa huku wakisema kuwa mimi ndio namjua aliyemuibia huyo Dimpoz.
Msanii LORD EYEZ
Katika hayo magari matatu waliyokuwa nayo halikuwepo gari la polisi na sikukamatwa na polisi ni raia walinishikilia muda mrefu sana bila kunipeleka polisi huku kuonyesha kutoelewana hata wenyewe na jioni kunipeleka kuliona gari lililoibiwa na kukuta watu wa kupiga picha wameandaliwa.
Hapa alikuwa ktk eneo la tukio la Dimpoz kuibiwa
Amesema kuwa anajua kuwa tu ni visa, na hii ilianzia kuwa kuna mtu nilionekana nae kuwaanahusika na hilo.

Na kama ikitokea kuwa kesi imeisha na kukutwa sina hatia nitakuja kuwaambia nitakachoamua. Kwani kwa sasa siwezi kuongea mengi kwani mengi ni ushahidi na kesi inaendelea.

Pia kuhusu Ray C, Amefurahi sana na kusema kuwa Mungu kafanya miujiza yake na pia Ray C ni rafiki yangu kama mwanzo.

Dec 20, 2012

ALICHOSEMA SUGU FACEBOOK, KIPO MAHAKAMANI LEO, DACTARI MBARONI KWA RUSHWA YA LAKI 1


Baada ya siku nyingi kupita, Mh. Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi "Sugu" Aliandika jana ktk ukurasa wake wa FaceBook kuwa anatangaza vita na madactari baada ya mara zote kuwatetea bungeni kutokana na vitendo vya rushwa ktk kitengo cha mifupa Rufaa Mbeya.
Sugu aliandika kwa herufi kubwaa.. ""NATANGAZA VITA NA MADAKTARI: MARA ZOTE NIMEKUWA MSTARI WA MBELE KWA KUTETEA HAKI NA MASLAHI YA MADAKTARI WETU BUNGENI,LAKINI KWA NIABA YA WANANCHI WA MBEYA LEO NATANGAZA VITA NA MADAKTARI WA HOSPITALI YA RUFAA-MBEYA KITENGO CHA MIFUPA,WAMENICHOSHA KWA RUSHWA AMBAYO IMEKITHIRI KAMA AMBAVYO SIJAWAHI KUONA MAHALI POPOTE.WANANCHI MASKINI WANALAZIMISHWA KULIPA TSHS 300,000/= MPAKA TSHS 500,000/= KWA AJILI YA KUWEKEWA JUST A 'P.O.P', AU VINGINEVYO MGONJWA ANAAMBIWA ANA TATIZO KUBWA LINALOHITAJI OPERESHENI NA KWAMBA AENDE PERAMIHO AU MUHIMBILI-DAR...KUNA TAARIFA KUWA KUNA WANANCHI WENGI WAMEKUFA NA WENGINE KUKATWA MIKONO NA MIGUUU KWA KUWA TU HAWAKUWA NA FEDHA ZA KUWAPA MADAKTARI HAO WA RUFAA-MBEYA...SASA KWA KUWA NIMEJARIBU SANA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI AKIWEMO RC MH. KANDORO BILA MAFANIKIO KWA MADAI KUWA HAKUNA USHAHIDI,SASA WAKIENDELEA KUKAA KIMYA NA WATU WETU WANAENDELEA KUTESEKA NA KUFA BASI TUTALAZIMIKA KUTUMIA NGUVU YA UMMA KUJITETEA KAMA KAWAIDA YETU""
Kiilichotokea leo ktk mahakama kuu ya Mbeya ni kuwa Daktari bingwa wa kitengo cha upasuaji akamwatwa na rushwa ya shilingi laki moja, afikishwa mahakamani leo..
Daktari huyo akifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza..
Habari kamiliitawajia hapa baada ya kesi kumalizika hapahapa..

Dec 19, 2012

HII NDIO TRAILER YA MOVIE YA OSAMA


MAKAMUA: KAZI YA QJ NI KUCHOMELEA

Rafiki mkubwa wa QJ ambaye pia ni msanii, Makamua, amefunguka kuhusu rafiki yake na kazi anayoifanya kwa sasa kuwa ni ya KUCHOMELEA.

Makamua akiongea “ni kweli QJ karudi kwenye hiyo kazi lakini ni sawa tu pia mi sioni kama kuna tatizo, sasa hivi anajipanga manake anataka kufungua sehemu yake yeye mwenyewe kwa sababu amekua akifanya kazi kwa watu, hata sisi tumemshauri ajiajiri mwenyewe kwa sababu ndio kitu ambacho anakipenda, sasa hivi anafanya kazi kwenye ofisi ya mtu”
Makamua na QJ kwa Stage..!
QJ alitangaza kuokoka na kuachana na bongofleva na kuthibitisha rasmi kwamba kwenye muziki wa gospel ndiko atakakosikika sasa hivi ambapo Makamua pia amesisitiza kwamba kazi kubwa anayoifanya QJ sasa hivi ni hiyo ya kuchomelea vyuma.

Kwenye mistari mingine pia Makamua amekanusha kuwa na uhusiano mbaya na staa mwenzake wa R’n'B ambae ni mshindi wa tuzo ya KTMA Ben Pol, kasema hakuna ukweli wa hizo taarifa na hata hivyo wamekua na maongezi ya kufanya single pamoja...

NU VIDEO, DIAMOND - KESHO


Dec 18, 2012

ANGALIA VIDEO MPYA YA BARNABA ILIVYOKUWA IKIANDALIWA NA ADAM


WEUSII FUNGA MWAKA

Fahamu kwamba baada ya rapper Lord Eyes kupata tuhuma za wizi wa vifaa vya gari la Ommy Dimpoz ni watu wengi wamekua na hamu ya kujua ataongea nini na atafanya nini kwenye siku yake ya kwanza kwenye stage toka hiyo ishu itokee.

Hajaonekana kwenye stage yoyote mpaka sasa na tayari kwenye Exclusive interview na millardayo.com alisema ana nyimbo tatu kichwani kuhusu yote yaliyotokea toka apate hizo tuhuma za wizi, na aliahidi pia kwamba december hii ndio ataachia single moja kati ya hizo.

Time imefika sasa hivi manake Weusi wanataka taarifa ikufikie kwamba stage ya Maisha Club december 23 2012 itamilikiwa na wao kwenye ‘Funga mwaka la weusi’

Kuna sababu kubwa za wao kuwa kwenye stage usiku huo, kwanza ni utambulisho wa single mpya ya Lord Eyez, ishu ya pili ni uzinduzi wa Bum Kubam DVD ya Nikki wa II ambapo G NAKO, JOH MAKINI,  NIKKI WA PILI,  BONTA na LORD EYEZ stage itawahusu kwa kadi ya mwaliko utakayoichangia elfu 10 tu.

DIAMOND NA VIDEO MPYA KENYA

Yeap!! That true Star anaeng'aa kwa sana hivi sasa nchini Tanzania, Diamond Platnumz a.k.a Rais Wa Wasafi anarekodi video ya ngoma yake mpya inayojulikana kama KESHO... what a simple title!!

Diamond anaetamba hivi sasa na track + video ya Nataka Kulewa na nyinginezo za nyuma, katika hali ya kuleta utofauti u kufanya video kali zaidi, anarekodi video hiyo huko Nairobi, nchini Kenya. Kesho ni video mpya inayofanywa ana Diamond ambayo pia itawaonesha mastaa mbali mbali wa nchini humo...

Dec 10, 2012

Ray C: ASANTE RAISI

Ray C, Akiwa na raisi wa Tanzania Mh. J. M. Kikwete
Msanii wa kike wa kizazi kipya, Rehema Chalamila maarufu kama Ray C, amemshukuru sana raisi kwa kumsaidia kupona kwake.

Ray C ni moja kati ya watu waliokuwa waathirika wa madawa ya kulevya kupelekea afya zao kuwa mbaya..
Kushoto ni Bibi, Mh. Raisi, Ray C na Dada..

DARASA. SikatiTamaa-MovieTrailer


WALTER CHILAMBO EpiqBSS NDANI YA AFTER XUL BASH 2012


Dec 9, 2012

Beauty na kaka zake wamepata kipaimara jana 08/12/2012

Baraka BOSCO, Beauty DANIEL na Nelson CHIFITA..
Brother Faraja naaa.........
Wakibarikiwa.
Tulivalishana mataji hadi baaaasiii
Pamoja sana..
Abby na dadaz
Beauty wiC her Friends..

Dec 7, 2012

ALICHOKISEMA MBASHA BOY KUHUSU SUGU NA WIMBO WAKE MPYA

"Hakuna matata ya Sugu ni moja kati ya ngoma kali za HIPHOP ambapo napenda kumpongeza sana kwa kazi nzuri hiyo" Alisema Mbuza..

Pia alimpongeza sana Sugu kwa kuwakuwakumbuka wakazi wa jiji la Mbeya na vijana kwa ujumla katika nyanja zote..
Allen Mbuza (Mbasha Boy)
Mr. II Sugu
Mtangazaji huyo wa kituo cha redio cha Sweet FM, Mkoani Mbeya, Mbasha Boy (Allen Mbuza) ambaye kwa sasa yupo Dar ktk masomo aliongea hayo kwa njia ya simu na mhariri wa blog hii na kutoa pongezi hizo..

Sionekani sana Dar sababu nakuwa jimboni, ni moja kati ya Punch line alizozipenda..

POLENI SANA NZOVWE

Moja kati ya Daladala zilizogongwa ktk eneo la tukio.
Mtu mmoja amekufa papo hapo na wengine kujeruhiwa katika ajali iliyotokea maeneo ya Nzovwe ambapo Roli limegonga daladala Mbili..

Dec 5, 2012

PIGO NIGERIA, RIP ELEBUWA

Mwigizaji nguli toka nchini Nigeria Enebeli Elebuwa (65) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo huko nchini India kutoka na ugonjwa wa kupooza uliompata mwaka 2011.

Alianza kuigiza mwaka 1967 na alikuwa anavutia sana akiigiza kama mfalme au 'pedeshee' na filamu nyingi ameigiza hivo.
Hizi ni baadhi ya filamu alizowahi igiza Lost Kingdom, Abuja Connection, Sensational, Dons in Abuja, The Corridors of Power, Men Do Cry, Who Will Tell The President, and Royal War.

Dec 2, 2012

KIMIRO STAR MAISHA PLUS

Mwanadada Bereniki Kimiro (Your New Maisha Plus Star)
Bereniki Kimiro ndiye ametangazwa kuwa mshindi wa Maisha Plus kwa mwaka 2012 kwa kuwashinda wenzake.

Nafasi ya pili imechukuliwa na Venance Kimaro na nafasi ya tatu imekwenda kwa Justine ambaye anatoka mkoani Dodoma.