Dec 20, 2010

Bashir asalimu amri kuhusu kura ya maoni

Rais wa marekani Barrack Obama ametangaza kuwa swala la Sudan ni mojawepo wa ajenda kubwa ya mashauri ya nchi za kigeni ya serikali yake.
Msemaji wa Ikulu ya White House Mike Hammer amesema bwana Obama amekwishawaandikia barua viongozi wa Afrika akiwataka kuunga mkono kura ya maoni kuhusu uhuru wa Sudan Kusini itakayoandaliwa kwa njia ya amani.
Awali rais wa Sudan, Omar al-Bashir, alisema Sudan Kaskazini itaimarisha sheria za kiislamu ikiwa Sudan kusini itapiga kura ya kujipatia uhuru.
Rais Omar Bashir.
Bwana Bashir amesema kwamba ikiwa taifa hilo litagawanywa, katiba ya Sudan itabadilishwa , Kiarabu itakuwa ndiyo lugha ya pekee, dini ya pekee itakuwa ni Uislamu, na sharia ndiyo katiba ya pekee itakayotumika nchini humo.
Mwandishi wa BBC mjini Khartoum amesema maneno ya bwana Bashir yanawatia hofu raia wa Sudan Kusini ambao si waislamu na ambao wanaishi Kaskazini.
Katika mkataba wa amani wa mwaka 2005 uliomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe, raia wa Sudan Kusini walilindwa dhidi ya makali ya sharia.

Dec 6, 2010

Wagombea wote waapishwa urais Ivory Coast

Ivory Coast iko katika janga kubwa la kisiasa, baada wa wagombea wote wawili wa urais kujiapisha kuongoza nchi.
Gbagbo
Laurent Gbagbo akila kiapo

Rais anayetetea kiti chake Laurent Gbagbo amekula kiapo cha kuongoza muhula mpya, lakini saa kadhaa baadaye Alassane Ouattara pia akala kiapo.
Marekani, Umoja wa Mataifa na Ufaransa zimesema Bw Ouattara ndiye ameshinda uchaguzi huo.
Bw Ouattara alitanagzwa mshindi la Tume ya Uchaguzi, lakini matokeo hayo yalitenguliwa na Baraza la Katiba, ambalo linaongozwa na mshirika wa Bw Gbagbo.
Uchaguzi wa raindi ya pili ya urais, ulikuwa na lengo la kuliunganisha taifa hilo ambalo ndio mzalishaji mkubwa zaidi ya kakao duniani, baada ua kuzuka vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2002.
Watu wasiopungua wanne wamekufa kuhusiana na ghasia za uchaguzi wiki hii, katika mji wa Abidjan.
Mitaani wafuasi wa upinzani wanaandamana wakipinga hatua ya Bw Gbagbo, wakisema hayo ni mapinduzi.
Wafuasi wa Bw Gbagbo wanasisitiza kuwa Umoja wa Mataifa hauna haki ya kusema nani ni mshindi, na wametishia kuwafukuza wafanyakazi wapataoo 8,000 wa umoja huo.

Dec 1, 2010

China yawaza uhusiano na Korea Kaskazini

Ripoti za mawasiliano ya siri kati ya balozi za Marekani zilizochapishwa kwenye mtandao wa Wiki Leaks, zinaashiria viongozi wa China wamekuwa wakifikiria ni nini kitafanyika iwapo uhusiano kati yao na Korea Kaskazini utasambaratika.
Kiongozi wa Korea Kaskazini alipokuwa China
Kiongozi wa Korea Kaskazini alipokuwa China

Afisa mmoja mwandamizi wa serikali ya Korea Kusini, aliwanukuu wawakilishi wawili wa China wakisema, Beijing itakuwa tayari kukubali ushirikiano wa karibu kati ya Korea Kusini na Kaskazini bora tu usihatarishe uhusiano uliopo na China.
Afisa mwingine wa China alinukuliwa akisema Korea Kaskazini imeedekezwa sana, matamshi yanayoonesha nchi hiyo imechoshwa na jinsi taifa hilo linavyoendeleza shughuli zake.
Kufikia sasa hata hivyo China imesema machache kuhusiana na kuchapishwa kwa nyaraka hizo za siri kwenye mtandao wa Wikileaks, lakini imekuwa ikiishinikiza Marekani kuhakikisha inachukua hatua mwafaka.

Wakazi Mogadishu hawawataki Al Shabaab

Matokeo ya utafiti wa kura ya maoni iliofanywa mjini Mogadishu, kwa niaba ya BBC, yamebainisha robo tatu ya wakaazi wa mji huo, hawataki wapiganaji wa kundi la Kiislamu wa Al Shabaab, kutwaa uongozi wa Somalia.
Maandamano ya kupinga kundi la Al Shabaab
Maandamano ya kupinga kundi la Al Shabaab

Uchunguzi huo umeonesha wengi wa wakaazi wa Mogadishu wanaamini kuwa kundi la Al Shabaab ni la kigaidi.
Wengi wao wahisi kundi hilo ni la upinzani. Asilimia hamsini ya wakaazi wa mji wa Mogadishu wanasema jamii ya kimataifa imelipuuza taifa lao ambalo halijawa na serikali kwa karibu miaka ishirini.
Utafiti huo umeendelea kuonesha asilimia tisini na mbili ya wakaazi wa mji huo hawana uwezo wa kukidhi mahitaji muhimu na ya kimsingi kama chakula na ulifanywa katika maeneo yanayodhibitiwa na kundi hilo la Al Shabaab.