Sep 16, 2012

WALTER KUINGIA MJENGONI EBSS NA WENZAKE 19


DITTO TUZONI

Msanii wa Bongo Fleva Lameck Ditto wa THT ametajwa katika wasanii wanao gombania Tuzo za Radio France International Discoveries kutoka Ufaransa .Kwenye hii tuzo wasanii kumi kutoka Africa huchaguliwa na kupambanishwa ,Ditto ameingizwa kwenye tuzo hizi kupitia nyimbo tofauti kama Wapo na Mi Amini na mshindi wa Tuzo hii atapata Euro Elfu kumi na mkataba wa kufanya show za live katika nchi 18 duniani.
Maeneo ya show hizi yatakuwa Afrika magaribi ,Marekani na Europe, Mkataba huu pia una kipengele cha promotion atakayo fanyiwa na Vituo vya Radio France. Nia ya Radio France kufanya Tuzo hizi ni kutangaza mziki wa Africa Duniani na mshindi wa kwanza wa tuzo hii kutoka Africa Mashariki alikuwa Maurice Kirya 2010 ,alishinda Euro 18,000 na kufanya show Mjini Paris na Tour ya Africa Ya Mwaka Mzima.

Sep 10, 2012

UZINDUZI WA VIDEO YA BAADAE YA OMMY DIMPOZ NDANI YA MAISHA CLUB

Usiku wa kuamkia leo msanii anayeshikilia tuzo mbili za Kilimanjaro Ommy Dimpozi alikuwa akizindua video yake mpya inayokwenda kwa jina la BAADAE ambayo location zake zilichukuliwa Joz South Africa na video kuzinduliwa Bongo ndani ya New Maisha Club kiwanja cha nyumbani.
Wasanii wenzake walikuwepo kumsindikiza Ommy Dimpozi, msanii kama Chege Chigunda alikuwa mmoja kati ya wasanii  waliofanya poa sana na kupata shangwe nyingi hadi kufikia time ya Ommy mwenyewe kupanda katika steji ya Maisha Club

Sep 7, 2012

BAADA YA KURUDI, NOKIA DON'T BREAK THE BEAT WANASEMAA,,,,,,,,


Ali aka Robin na Njama Ndio walio shine zaidi Tanzania na kwenda kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Freestlye kupitia Nokia Dont Break The Beat.Mobi.

Mshindi wa nne alitoka Tanzania nae ni Njama na wapili ni Ali aka Robin. Baada ya Njama kurudi Tanzania ametangaza kwamba anatafuta lebel au deal ya kufanya kazi na producer yoyote Tanzania atakaye ingia mkataba nae .

Pia amesema anawakubali ma producer kama Duke wa M Lab,Lamar na Tongwe Records, na Alivyokuwa kenya alikutana na Cannibal na tayari wana mpango wakufanya collabo.

Ali kwa sasa tayari amesha fanya nyimbo kadha na zipo studio  zikifanyiwa final mixing na pia amefunguka kuwa kufanya kazi na Belle 9 ni kitu anacho taka kufanya baada ya kukamilisha project zake za kwanza .

HUYU NDIO MWANAJESHI ALIYEANDIKA KITABU KUHUSU OSAMA

Wizara ya usalama ya Marekani (Pentagon) imetishia kumpeleka mahakamani mwanajeshi alieandika kitabu kuhusu jinsi yeye na wenzake walivyomuua gaidi Osama Bin Laden aliekua kiongozi wa Al Qaeda.
Mwanajeshi huyo aliekua kwenye kundi la wanajeshi wenye ujuzi wa hali ya juu alikua mtu wa pili kuingia chumbani alipokuepo Osama ambapo kwenye kitabu alichoandika anaeleza kwamba Osama hakua na silaha yoyote walivoingia chumbani kwake, taarifa ambayo inatofautiana na iliyotolewa na Pentagon.

Kanuni zinazoongoza oparesheni kama iliyomuua Osama zinawanyima wanajeshi waliohusika kutoa siri au kutangaza chochote ndio maana anaonekana kavunja makubaliano.

Sasa hivi vyombo vya habari vimeanza kuhusisha hicho kitabu na kampeni za urais jambo ambalo mwanajeshi huyo amelikataa na kusisitiza kwamba amekiandika hicho kitabu ili kuweka hadharani ukweli bila kulenga chama chochote cha siasa wala mgombea.

Matt Bissonnette(36) ambae hafurahii uongozi wa rais Obama, alikua hataki kutambuliwa kwenye vyombo vya habari lakini tayari jina lake limeshajulikana na limesambaa hivyo ilimlazimu kujificha.

Sep 6, 2012

FUNDI SAMWELI KUSEPA BONGO, HARUDI TENA

Yule Producer mkali kutoka pande za Kibaha Fundi Samweli amenitumia msm iliyokuwa inasema hivi
"Mpendwa mteja nitaondoka Tanzania mwezi wa 10. Sitorudi tena nitamwacha Producer wangu Zidady studioni, ataendeleza kazi yangu namba yake ni 0719 868085
Fundi Samweli"

BAGHDAD KUENDESHWA, APEWA RATIBA YA KUISHI

Pray god kweka almaarufu kama Baghdad amesimamishwa kwa kipindi kisichojulikana kufanya baadhi ya mambo. Kauli hii imetoka kwenye management ambayo inamshikilia msanii huyo ambae hivi karibuni9 tuu tulisikia amepata shavu la kuwa chini ya studio kubwa nchini marekani chofacho rec amezuiliwa kufanya show, collabo,intaview,movie,N.k na kupangiwa rasmi ratiba yake ya kila siku italkayomfanya yeye kufanya kazi iliyokusudiwa na mangment. 
Daudi lucas alieleza ya kuwa Baghdad ametumiwa ratiba ndefu saana ya kurecord nyimbo zake ukiangalia anatakiwa atunge ngoma kuanzia 5 mpaka 12 kwa kipindi hichi kifupi video zaidi ya tatu kabla mwaka huu haujaisha, na kama unavyojua aliwahi kuuguwa ugonjwa wa kisukari mazoezi anayotakiwa ni mazito saana na jaaana tuuu tulikuwa dragon kwa ajili ya kumtafutia pumzi kwa njia ya kuogelea na kumbe cha kushangaza alikuwa hajui hata kuogelea sooo tunajitahidi kukimbizana na muda na kuziba baadhi ya mapungufu ya Baghdad na hata choka nadhani unakumbuka siku niliomleta kuja kushot pamoja we can alikuwa hawezi kutembea vizuri kwa sasa amebakiza asilkimia chache saana ili kurudi mwendo wake wa zamani sooo tukagundua tunahitajika kumuweka mbali na club, show, colabo, hata intaview ili asifikirie kitu kingine zaidi ya kujiandaaa kwa kuwa intanational artist” baada ya kuyasema hayo niuliamua kumuuliza vipi kuhusu vipindi vyake vya tv? Daudi lucas “ratiba tuliyompa huwa anapata masaa 8 ya kupumzika 4 ya kufanya kazi na sikku za week end huwa tumempa ruhusa ya kuchukua usafiri na kwenda kutembea na girlfriend wake nay eye alituomba ya kuwa ana vipindi vyake anavyohitaji kuvishoot well tulimuelewa kwa kuwa tunapenda afanikiwae na we happy all the tym tukamwambia apange sikui atakayokuwa anashoot kisha atuambie nini anahitaji we will do it for him sooo ni yeye kutumia muda wake wa ziada badala ya kuutumia saana kuwa na mwenzi wake anaweza kujiiba kwa muda hata wa siku moja kati ya 2 tulizompa kuwa free tangu asubuhi mapka jioni na kizuri kutoka kwa mpenzi wake sio mbish anamulewa saaana 
Baghdad na anapenda kumsikiliza so hilo halitakuwa na matatizo nadhani na haliingiliani kabisa na utaratibnu wake wa ki mziki” niliomba kuwa wa mwisho kumuhioji Baghdad na nilipewa ruhusa ya kumuhoji na naamini mimi ndie nitakuwa wa mwisho kumuhoji kwa sasa nilimuuliza Baghdad anaonaje kuwa under mangment. baghdad“ unajua ilikuwa ni ngumu saana mi kuwa na management ingawa nyingi tuu ziliwahi kunihitaji ila nilichokuwa nakikataa huku hakipo, so najisikia poa sana kuwa chini ya management. 2. 
Umepokeaje kali ya kusimamishwa kufanya baadhi ya vitu “ mwanzo niliona wananizogoa ila uwezi amini kwa sasa najiona mpya kwa kuwa sina stress yoyote zaidi ya kutunga tuuuu! 3. Una lolote kwa kuwa hatutaongea tena kwa muda usiojulikana “ daaa watu wangu wasinie,lewe vibaya watangazaji watakaoniita kwenye intaview nikikataa wasinbielewe vibaya, wadau wa mziki nia ya kufanya hivi ni kuandaa kitu kizurio so nawaombeni kwa lolote msiache kuniambia na mimi nitalifikisha kwenye mangment yangu page yangu ya mwanzo fb imejaa so wanicheki kwenye pag mpya Baghdad pg wasiweke kweka waniambie lolote ila kwa intaview, collabo wapige kwenye 0716 89 00 85 wataongea na management.  Stop……………. Kufanya intaviews, colabo, shows, movie, hata kunaniliu na naniliu wake nayo stoooop Baghdad ekheee nakutakia ,mafunzo mema ya kuogelea ukishajua niambie tushindane!

IZZO B: NIPO KIBIASHARA, MBEYA ALL STAR SIHUSIKI

Rapper Izzo Buzness amefunguka kuhusu Mbeya Allstars na kusema hakujua kuhusu hio nyimbo wala imetengenezwa wapi na hajahusishwa.

Izzo amesema kuwa hajakataa kufanya Mbeya All Stars ila kwa sasa huu mziki ni biashara na kila unachifanya uwe na malengo sio ku copy na ku paste tu. 

“Kigoma All Stars wamefanya kitu kizuri na wame safiri kwenda Kigoma na Wamefanya show, Pia wameboresha mambo yao tofauti kupitia udhamini wa hio nyimbo, Wakati unafanya Project kama hizi lazima ujue lengo lako na sio kufanya tu….”

Izzo alisema Tayari watu wa Mbeya wanajua anachofanya na anawakilisha vizuri kabisa na hilo ni tosha kabisa kwa mji wake…

“Sio sababu wao wamefanya na sisi tufanye ila kuna mambo ya muhimu zaidi ya kufanya mziki.”

MANECK: SINA BIFU NA MARCO CHALI


Producer Maneck ambae ni mshindi wa tuzo kwenye KTMA 2012 ameamua kuzungumza ya moyoni kwa kuijibu kauli Dogo Janja aliyoitoa kwamba Producer huyo kauponda uwezo wa Marco Chali.

Ishu ilianza wakiwa club Maisha Dar es salaam jumapili iliyopita ambapo Dogo Janja anadai alikwenda sehemu ya V.I.P na kumsalimia Maneck ambae hakujibu salamu ila aliporomosha matusi mazito kwa Dogo Janja pamoja na kumpiga biti kwamba asimsogelee.

Baada ya hapo Dogo Janja akashuka chini kwenda kumwita meneja wake wa WATANASHATI ambae ni Ustaz Juma ambapo kwa maelezo ya Dogo Janja, Maneck alianza kuiponda single mpya ya Dogo Janja na PNC waliyoirekodi kwa Marco Chali ambayo mwanzoni ilikua irekodiwe kwa Maneck alieiponda kwa kusema ni ya kawaida sana kwa sababu imefanywa na Marco Chali.

Jibu alilolitoa Maneck baada ya kusikia kwamba Dogo Janja amenukuliwa kwa hayo maneno, namkariri akisema “ndio ninavyokwambia sitakagi watu masnich kama huyo, Marco Chali ni mtu ambae namfil sana anafanya kazi nzuri, siwezi kuongea kitu kibaya kwa Marco kwa sababu leo na kesho nitamfata nitamuomba msaada wa kitu chochote kile hata material sasa nitawezaji kusema hivyo kwa mfano sasa, Dogo Janja ni mtu ambae anataka tu kufanyaga vitu watu wapishane kauli mambo ya kijinga ni utoto akikua nadhani ataacha hizo tabia zake, na ndio maana nikamwambia kaa mbali sitaki uongee na mimi that’s all”

Sep 4, 2012

PICHA ZA IZZO B KATIKA VIDEO YAKE MPYA

UGOMVI MANECK, TUNDA NA DOGO JANJA

Maelezo ya Dogo Janja yanaamplfy kwamba juzi (September 2) walivyokua Club Maisha aliperform akiwa na furaha kutokana na mashabiki zake waliojitokeza na alipomaliza kuperform alishuka kwenye stage akiwa na furaha baada ya kufanya vizuri lakini hiyo furaha ilikatishwa baada ya kwenda juu sehemu ya V.I.P.

Janja anasema alipopanda V.I.P kumsalimia Producer Maneck alimjibu kwa dharau na kumwambia haongei na Masnich hivyo Dogo Janja akaondoka lakini muda mfupi baadae alirudi na kukuta Tunda Man yuko karibu na alipokaa Maneck, Janja pamoja na Tunda walimsogelea producer huyo ambae alianza kumtukana matusi mazito Dogo Janja.

Baada ya hapo ilibidi Dogo Janja kushuka chini na kwenda kumchukua Ustaz Juma ambae ndio boss wa kundi alilopo sasa Dogo Janja la Watanashati, walipofika alipo Maneck.. alianza kuiponda single mpya ya Dogo Janja aliyorekodi na producer Marco Chali kwa kusema wimbo huo ambao mwanzo ulikua urekodiwe kwa Maneck ni wa kawaida sana.

Maneck na Tunda Man.

Kwenye line nyingine namkariri Dogo Janja akisema “nikawa nimepanic sana sasa leo nakuja kupokea simu eti Tunda man nae anasema nifute chorus ya ‘Anajua’ kwenye wimbo wangu, Bro ule wimbo nimeurekodi nikiwa Tip Top na nimeifanyia show nyingi sana Tanzania ambazo zimewaingizia hela nyingi sana, hawana ubinadamu yani wanaponiambia mimi nifute chorus, Tunda kawafanyia watoto wangapi chorus? Shetta, Pasha lakini mbona hamwaambii Pasha afute au labda sababu mi mdogo, hili swala nawaachia watanzania kwa sababu ile ni haki yangu, nilimshirikisha Tunda.. ule wimbo sio wa Tunda siwezi kufuta chorus”

Baada ya hayo maelezo ya Dogo Janja, Producer Maneck amezungumza exclusive na millardayo.com na namkariri akisema “Dogo Janja alikuja akanisalimia nikamwambia ebwana eeeh kaa mbali na mimi sihitaji kuongea na wewe kwa sababu unatabia za kisnich sana, kuna vitu flani alivifanya siku kadhaa zimepita na sikupendezwa navyo.. tuliandaa show ya Tunda Man pale Maisha Club  tukamwambia na akakubali kufanya na tukatangaza kwamba atakuepo sasa mwisho wa siku akabroadcast msg kwenye BBM alafu sisi hakututumia ile msg ila akabroadcast kwa watu kwamba hao ni matapeli, hapohapo nachat nae namuuliza mbona umezingua anasema mi naona aibu sijui hata sura yangu sijui nitaiweka wapi kwa bwana Captain, huku anasema hivi huku anafanya hivi”

Tunda Man nae ametoa sababu za kumwambia Dogo Janja afute sauti yake kwenye kolabo waliyofanya ya ‘Anajua’ na nina mkariri akisema ” sikuzungumza kwa ubaya, nimezungumza kwa nia nzuri tu.. kwenye chorus inasema niko na Captain Tunda man alafu mimi siko pale mashabiki wanakua kama hawakuelewi vizuri, kuna mistari mingine inasema narun city nikiwa na JCB, narun Dar City nikiwa na T.I.P sasa ujue kwenye show kuimba vitu kama hivyo wakati hayupo na Tip Top vinakua havileti maana, ni kama maoni tu nimemuomba aimbie beat  kwa sababu anaweza kurekebisha ile mistari, mfano kusema narun city nikiwa na Watanashati, kwenye show ndio abadilishe lakini kwenye audio ni sawa ikibaki na vionjo vya mwanzo”

WALTER ASHUKURU MUNGU KUPENYA EBSS

Msanii wa kizazi kipya mkoa wa Mbeya, Eric aliyefahamika kwa jina la SpeechWise ambaye jina lake la kwenye cheti ni Walter Chilambo, ameanza safari mpya ya muziki baada ya kupenya kuingia katika 50 bora za washiriki wa EBSS kutoka katika mikoa mbalimbali Tanzania nzima.

Amezungumza na abbynm5.blogspot.com baada ya kile alichoandika katika FaceBook kuwa anamshukuru Mungu kufikia hatua hiyo kwani kwa idadi ya watu waliohudhuria Coco na vipaji vilivyokuwepo na kupenya katika 50 bora.

Pia Walter amesema kuwa kwa uweza wa Mungu anatarajia kufika mbali sana katika mashindano hayo ikiwa ni pamoja na kuifikia na kuikwapua zawadi ya mashindano hayo ambayo ni fedha za kitanzania Shilingi 50,000,000/=.

Katika status hiyo, Walter alisema "Kwa nyomi lile la Coco beach hadi kuingia 50 bora kukutana na wengine kutoka mikoani ni bonge la hatua.. Au sio wangu......" na watu kibao walimpongeza kwa hatua aliyofikia..
 Pipo walivyokuwa Coco.
KILA KILA LA KHERI KATIKA HILO WALTER.

Sep 3, 2012

PICHA ZA DIAMOND AKILA BATA NA DANCERS WAKE WASHINGTON DC MAREKANI

WAANDISHI MBEYA WALAANI MAUAJI YA MWANGOSI

WAANDISHI na Wanachi mkoani Mbeya wamelaani vikali Mauaji ya Mwandishi wa habari wa Iringa Daudi Mwangosi,  aliyeuwawa Janai katika vurugu zilizotokea katika kijiji cha Nyororo mkoani humo.

Marehemu Mwangosi ambaye alikuwa ni Mwenyekiti wa Klabu yawaandishi wa habari mkoa wa Iringa pia alikuwa akifanya kazi katika kituo cha Chanel Ten aliuawa wakati akiripoti vurugu zilizotokea kijijini hapo baina ya  Chadema na Polisi.

 Huyu ni Mwenyekiti wa Chama Cha waandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya,
Christopher Nyenyembe.

IZZO-B VIDEO SOON, MBEYA ALL STAR WATISHA

Izzo Bizness msanii wa hip hop kutoka Mbeya, baada ya kuachia video ya MWAKA JANA sasa yuko tayari kabisa kuachia video nyingine ambayo imebeba jina la UTARUDISHWA ambapo ndani ya wimbo huo amemshirikisha msanii kutoka Morogoro
Belle 9.


Video hii imetengenezwa na yule yule Director ambaye alifanya video ya mwaka jana anajulikana kwa jina la Nick Dizzo kutoka E-Media.

Wakati huo huo, wasanii kutoka Mbeya (Mbeya all star) wameachia bonge la video likisifia Green city ambayo imetengenezwa na Mashada inc, production kutoka Mbeya..

Kuangalia video ya Mbeya all star tembelea blog ya DJ Choka...................

PICHA ZA MWANDISHI ALIYEUAWA NA POLISI IRINGA

 
 Inaonesha Polisi walishajipanga, si unaonaaa hapo juu..
Mwili wa Marehemu Daudi ukiwa chini baada ya kulipukiwa na bomu.

Sep 2, 2012

WALTWER WA EBSS KUFUNGUKA LEO ITV.. ASEMA KTK FACEBOOK

Angalia Usaili wa EBSS Dar leo jumapili ITV tym ya 9:30 PM. Kumbuka I am Walter Chilambo...

MARLAW AONGEA KUHUSU KUTOMPA MIMBA BESTA

Katika gazeti kubwa la burudani Tanzania la Baabkubwa lililotoka hivi karibuni ambalo husomwa na wabongo wengi wanaopenda stori za burudani kiliandikwa kichwa cha habari kwamba Marlaw ameshindwa kabisa kumpa mimba mkewe Besta ambae ni msanii pia.
 
Marlaw hapa amesema maneno 99 tu! Eti,,,  “Swala la mimi kumpatia mimba mke wangu au uzao wa familia yangu ni swala langu binafsi, sidhani kama ni swala la Baabkubwa, mi sijapenda alafu na dizaini walivyoelezea yani ile interview mimi ninavyozungumza yale sio maneno yangu...........kama walinipigia simu basi ningependa kama wangeandika kile hasa ambacho hasa mimi nimekisema, nakumbuka walishawahi kunipigia simu lakini tukazungumza lakini mazungumzo hayakua vile jinsi ilivyokuja kuandikwa, yamebadilishwa.....sitochukua hatua yoyote nataka tu wanipigie simu waniambie samahani, mtu ataenipigia simu anipigie tu tumalize tuongee tu yaishe, kama wangependa kuandika kwenye gazeti lijalo waandike kile nilikiongea”

Baada ya hayo nilipochek na Baabkubwa walikua kwenye kikao lakini wakasema time ikifika msemaji atazungumza...