Sep 4, 2012

WALTER ASHUKURU MUNGU KUPENYA EBSS

Msanii wa kizazi kipya mkoa wa Mbeya, Eric aliyefahamika kwa jina la SpeechWise ambaye jina lake la kwenye cheti ni Walter Chilambo, ameanza safari mpya ya muziki baada ya kupenya kuingia katika 50 bora za washiriki wa EBSS kutoka katika mikoa mbalimbali Tanzania nzima.

Amezungumza na abbynm5.blogspot.com baada ya kile alichoandika katika FaceBook kuwa anamshukuru Mungu kufikia hatua hiyo kwani kwa idadi ya watu waliohudhuria Coco na vipaji vilivyokuwepo na kupenya katika 50 bora.

Pia Walter amesema kuwa kwa uweza wa Mungu anatarajia kufika mbali sana katika mashindano hayo ikiwa ni pamoja na kuifikia na kuikwapua zawadi ya mashindano hayo ambayo ni fedha za kitanzania Shilingi 50,000,000/=.

Katika status hiyo, Walter alisema "Kwa nyomi lile la Coco beach hadi kuingia 50 bora kukutana na wengine kutoka mikoani ni bonge la hatua.. Au sio wangu......" na watu kibao walimpongeza kwa hatua aliyofikia..
 Pipo walivyokuwa Coco.
KILA KILA LA KHERI KATIKA HILO WALTER.