Nov 28, 2012

POLE ZAMARADI KUFIWA

ZAMA
Mtangazaji wa Clouds FM na Clouds TV (Take One), Zamaradi Mketema, leo hii amefiwa na mama yake mzazi aliekuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kansa kwa muda mrefu.

Tunakupa pole wewe pamoja na familia yako, Mungu akupe nguvu katika kipindi hiki kigumu.Eeeh! 

Mwenyezi Mungu ilaze roho ya marehem mahali pema peponi. AMEN.

Nov 26, 2012

Rest In Peace SHARO BILIONEA

Msanii, Muigizaji, Mchekeshaji Hussein Ramadhani aka Sharo Bilionea amepata ajali ya gari akiwa anaendesha mwenyewe Toyota Harrier akitoka Dar kwenda Muheza kwao.

Kamanda wa polisi mkoani Tangawamethibitisha kifo chake kutokana na vitambulisho alivyokutwa navyo pia taarifa kutoka kwa rafiki yake Diwani Seif Makame amesema ajali hiyo imetokea mida ya saaa Mbili leo...


Rest in Peace Brother..

Nov 18, 2012

AY AMEFANYA YAKE BONDENI

 Hongera nyingi sana kwa AY.
AY Running East Africa
Msanii wa Bongo Flavour almaarufu kama AY huko nchini South Africa amejichukulia tuzo ya kwanza katika kipengele cha Most Gifted East Africa Video of the Year.

C. NYENYEMBE: CCM WANATEGEMEA POLISI?

Na Christopher Nyenyembe, Mbeya.
Christopher Nyenyembe (TanzaniaDaima Mbeya)
HIVI leo, Rais Jakaya Kikwete na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) anapotamka hadharani kuwa CCM waache kutegemea polisi ana maanisha nini?

Sijui anataka kuwaambia nini Watanzania wa leo kuwa jitihada kubwa za kukijenga chama hicho na nguvu kubwa inayotumiwa na vyombo vya dola wakati wa uchaguzi mkuu, rais alikuwa haoni.

Sijui anatoa darasa gani kwa wana CCM wenzake kuwa waache tabia ya kuwategemea polisi katika harakati zao za kisiasa akisahau kuwa polisi ndio wanaotumika kuwasambaratisha wafuasi wa vyama vingine vya siasa vinapotekeleza majukumu yao ya kisiasa.

Kauli ya Rais Kikwete kama ilivyonukuliwa na vyombo vya habari mjini Dodoma wiki hii alipokuwa akifunga mkutano mkuu wa nane wa CCM, moja ya kauli yake ilikuwa kukionya chama anachokiongoza kuwa kisiwategemee polisi katika masuala ya kisiasa, kwa kuwa kufanya hivyo CCM watakuwa wakijidanganya.

Onyo hilo la rais kama mwenyekiti wa chama cha siasa anachokiongoza linatia shaka kwa kuwa naamini zuio hilo limetolewa muda ambao yeye binafsi anajua fika kuwa hagombei tena urais mwaka 2015.

Alikuwa wapi kuwazuia polisi waliowapiga mabomu wananchi wa mkoa wa Arusha wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2010, waliopigwa mabomu Mwanza, Mbeya, Morogoro, Singida na Dar es Salaam ili watu waogope kwenda kupiga kura.

Siamini na sidhani kama agizo la mwenyekiti wa chama hicho, ambaye ni kiongozi mkuu wa chama hicho kikongwe cha siasa kuwa ndiyo dhamira ya kweli ya kukitaka chama hicho kiache kutegemea polisi katika masuala yao ya kisiasa.

Sitaki kujirudisha kwenye maumivu makali ya kisiasa na namna polisi walivyoweza kutumika kuvuruga shughuli za kisiasa zinazoendelea kufanywa na vyama vya upinzani, hususan CHADEMA siku waliyofurumshwa na mabomu kule Nyololo, Mufindi, Mkoa wa Iringa.

Polisi hao walifanya kazi ya kutuliza vurugu ambazo hazikuwepo na hatimaye kusababisha kifo cha mwandishi wa habari wa Kituo cha Channel Ten, marehemu Daudi Mwangosi, katika tukio hilo niliamini fika kuwa katika kukemea nguvu kubwa inayotumiwa na polisi katika masuala ya kisiasa, Rais Kikwete angetoa pole kwa familia ya marehemu lakini hakufanya hivyo.

Nilisema na narudia kusema tena kuwa situmi ombi kwa rais kutaka kumwambia kuwa, watoto wa marehemu Mwangosi wanamlilia, na hata Mwangosi mwenyewe anamlilia anauliza Rais Kikwete uko wapi Mwangosi ninakulilia? Hayo yamepita, leo hii Mwenyekiti wa CCM anakionya chama chake eti kisitegemee polisi.

Kwa maana hiyo na matukio kadhaa yanayotokea dhidi ya vyama vya upinzani ambapo polisi walioajiriwa na serikali inayoongozwa na CCM kuwa ni kweli wanatumwa na chama hicho ili kuvidhibiti vyama vingine vya siasa vinavyotishia uhai wa CCM.

Iweje kama nguvu kubwa zimekuwa zikitumika kuvizima vyama pinzani ili kudhoofisha harakati zao za kujijenga, leo hii itawezekana vipi kama rais huyo huyo akiwa Mwenyekiti wa CCM taifa ameirudisha safu mpya iliyokuwa chini ya Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa na kuwataka viongozi hao wasitegemee polisi.

Yapo maswali ya kujiuliza kuwa enzi za kina Philip Mangula, Abdulrahaman Kinana, Seif Khatib na Mama Zakhia Meghji wakiwa kwenye safu ya Mkapa walikuwa hawategemei polisi ili kuendesha harakati zao za kisiasa na kama walikuwa wanategemea polisi wamerudishwa upya ili waache kutegemea polisi ?

Nauliza nikiamini kuwa uzoefu wa CCM wa kutegemea polisi katika masuala yake ya kisiasa ulianza lini, ulianza kabla ya mfumo wa vyama vingi vya siasa au ulianza baada ya kuanzishwa kwa siasa za vyama vingi ndipo CCM walipogundua kuwa polisi ni mali yao.

Na kama miaka yote CCM wanaamini kuwa polisi ni mali ya CCM na vyama vingine vya siasa havina polisi, kauli ya Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho aliyoitoa mkoani Dodoma ya kukionya chama chake kisitegemee polisi anataka kuwaambia nini Watanzania ambao bado wapo usingizini.

Lakini ni vema ninukuu kwa undani kile alichokisema juu ya CCM na utegemezi wa nguvu za polisi, kuwa kitendo cha wana CCM kuishi katika siasa kwa kutegemea Jeshi la polisi hakipaswi kukubaliwa kwa kuwa kimepitwa na wakati.

“Mnaishia kulalamika tu kila siku eti wanatukana halafu mnaishia kusema kawaida yao… au utasikia mtu anasema eti serikali haipo!Kazi ya serikali siyo hiyo, hiyo ni kazi ya kisiasa maana hao ndio wenzenu,” alisema Kikwete alipokuwa akifunga mkutano huo.

“Sasa mnataka wakisema serikali ya CCM haijafanya kitu,polisi wawafuate, au wakisema Kikwete nchi imemshinda, polisi wawakamate ? Kama wakisema hatujafanya kitu, ni kazi yenu kusema kwamba tumefanya kitu, waonyesheni barabara, shule na mambo mengine.

“Mkijibu kwa hoja wanatulia, siyo polisi. Nakumbuka Mwigulu aliwajibu pale bungeni kuhusu bajeti yao mbadala. Walipoitoa kijana wetu akasimama na kupigilia msumari kweli wakachanganyikiwa sasa hizo ndio kazi zinazotakiwa jamani,” alisisitiza Kikwete.

Kama, Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Kikwete ameamua kukiambia chama chake leo kuwa kisitegemee polisi, alikuwa wapi kukionya mara tu alipoteuliwa kwa mara ya kwanza kutoa kauli hiyo katika mkutano mkuu wa saba alipochukua mikoba iliyoachwa na rais mstaafu Benjamin Mkapa.

Nini kimetokea ndani ya CCM na safu yake mpya inayoelekea kwenye vuguvugu la uchaguzi wa mwaka 2015 huku kukiwa na zuio kubwa la kukitaka chama hicho kiendeshe masuala yake ya kisiasa bila kutegemea polisi, wameona hasara gani ya kutumia polisi.

Naamini kuwa mtaji mkubwa wa CCM katika medani ya kisiasa imekuwa ikielekezwa kwenye matumizi ya nguvu za vyombo vya dola siyo polisi pekee yao ambao CCM wanatakiwa waache kuvitumia, waache kabisa kutumia raslimali za nchi kwa lengo la kukijenga chama chao, waache ili serikali iwe salama.

Kama CCM wanaambiwa hivyo leo, basi Rais Kikwete hakuona alipokuwa akihutubia mkutano huo jinsi watendaji wa serikali walivyokuwa wamejazana Dodoma wakiwa ndani ya ukumbi wa Kizota, huku ni wakuu wa wilaya na mikoa na upande wa pili ni wajumbe wa kamati za siasa za chama hicho.

Watendaji wengi wa serikali wametumia kwa kiasi kikubwa raslimali za nchi na kulipwa masurufu kwa kazi za chama, mara baada ya mkutano huo kumalizika wamebaki Dodoma kwa kigezo cha kushiriki kwenye mrejesho wa semina elekezi kwa watendaji wa serikali hayo ndio maajabu ya CCM.

Rais Kikwete anapaswa kusoma alama za nyakati kuwa Watanzania wa leo hawaamini moja kwa moja mawazo ya mtu mmoja ili kuweza kuijenga nchi yenye utawala bora bila kukiuka misingi madhubuti ya haki za binadamu.

Kwa kuwa haki za binadamu zimekuwa zikikiukwa kwa misingi pengine ya kukibeba chama tawala ili kiendelee kushika dola hata kama wananchi wamechoka, rais alipaswa kuliagiza Jeshi la Polisi kuwa liache kuingilia masuala ya kisiasa na si kukiambia chama chake kuwa kisitegemee polisi, hilo si zuio ni agizo la kiutendaji kwa upande wa pili wa shilingi.

Naamini kuwa ili nchi iweze kujielekeza kwenye ujenzi wa demokrasia ya kweli ndani ya mfumo wa vyama vingi vya siasa, basi kila chama kinapaswa kuheshimu sheria za nchi na taratibu zote za kuendesha vyama vya siasa ili kuepuka vurugu.

Jeshi la Polisi nao wafanye kazi zao kwa mujibu wa sheria ili chombo hicho kisitafsiriwe kuwa ni mali ya CCM na ili kuondoa dhana hiyo polisi wamesikia, kuwa CCM sasa haitawategemea tena.

Nov 14, 2012

BEN POL, WALTER KUFANAYA BOONGEE LA COLLABO

Ben Pol Akimtuza Walter wakati anaimba Nikikupata nyimbo yake.
Msanii Ben Paul aliyeimba wimbo uliompa ushindi Walter wa Epic BSS amesema Alishaongea na Walter wakati wa kujitayarisha kwa ajili ya show ya fainali na kusema alimwambia Angependa kufanya kazi na Walter akiwa tayari kufanya kazi muda wowote.


Kwasasa ameshinda so achukue muda wake kujipanga ukizingatia kwa sasa watu wakaribu naye watakuwa wakimshauri sana.

Ila fahamu kuwa Ben Paul yupo tayari kufanya wimbo na Walter muda wowote.

Pia kuhusu Walter kuchagua `Nikikupata' kama wimbo wake wa mwisho kuimba nikitu kilicho mfurahisha sana Ben Paul na Ben amesema walivyo kuwa Back Stage Walter alimwambia ataimba wimbo huo kwenye show yake so Ben Paul alibidi autoe wimbo huo kwenye orodha ya nyimbo alizo taka kufanya kwenye show yake.

Kuhusu show aliyo fanya Ben Paul kwenye Epic BSS, Ben amesema tayari washindani walikuwa wamekaa kwenye mafunzo na walikuwa wanajua kufanya show nzuri ila kila msanii anauwezo tofauti na alichotaka kufanya nikuwaonyesha vitu na maujanja zaidi kwenye show ile ili wajifunza na waondoke na mambo tofauti kutoka kwa Ben Paul.

Nov 10, 2012

Angalia Video ya Walter baada ya Kutangazwa mshindi EBSS 2012


Mama mzazi wa Walter Chilambo akiongea na Watanzania juu ya ushindi wa mwanae


STAR: MJUE ALLEN MBASHA BOY MBUZA

ALLEN MBASHA BOY MBUZA ni DJ na Redio Presenter katika kampuni ya TMP Media ambayo inamiliki kituo cha rediio mkoani Mbeya (Sweet fm)

Allen pia yupo shule kwa sasa katika chuo cha Institute of Finance Management (IFM) ambapo anachukua Bachelor of Science in Social Protection kwa kipindi cha mwaka wa masomo 2012/14 pale jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Allen ambaye anishi kwao maeneo ya Soweto, Mbeya alimaliza elimu ya sekondary ya juu mwaka 2010 pale Sangu Sec. Mbeya.

Kama ulikuwa hujui pia Allen yupo katika mahusiano ya kimapenzi na mtoto ........... ambaye bila woga kamtaja katika ukurasa wake wa Facebook.


Akiwa ametokelezea.
Pia Allen ni mhusika katika kampuni ya  The mbuzax auctionmart and court brokers. Kama ukihitaji kuwasiliana na kumjua zaidi Star wetu wa leo mtafute kupitia  0716 763 571.

By Abby Mbungula. Mbeya.

Nov 9, 2012

JINSI WALTER ALIVYOSHINE

Mshindi wa pili Salma akiwa jukwaani kuonyesha uwezo wake
Mada akimuweka sawa jaji Master J.
Baada ya Washiriki 2 kutoka wakabaki Top 3, Yeye, Salma na Wababa.
Ben Pol akimtuza Walter wakati akiimba nyimbo yake-Nikikupata.
Wakisubiri kutangazwa mshindi baada ya kubaki wa2.
CCO wa Zantel akitaka kutaja MSHINDI.
Hii ndio top 5 iliyoperfom jana.
Madam akimjaji Walter
Baada ya kutangazwa mshindi, Walter ali... ni hisia za kutoamini
Alishikiliwa akikabidhiwa huku mchozi ukimshuka.
Akikabidhiwa zawadi, hata hakuamini machozi tuu.
Kumbe alipendwa sana tukiachana na mbwembwe za yule.
Washereheshaji.
Shabiki walikuwa nyomi.
Walter akirushiwa pesa jukwaani
Walter alipopanda stage na Ditto.

Walter Chilambo Baada ya Kutangazwa mshindi aongea na waandishi


MSHINDI WA EBSS 2012 WALTER

 WALTER Chilambo amekuywa mshindi wa Epiq Bongo Star Search kwa mwaka 2012/13 baada ya kutangazwa jana..

Katika mtandao wake wa Facebook Walter kaandika, "Asante sana Mwenyezi Mungu.
Nakushukuru Mama yangu, Baba. Asante kwako wewe uliyeniwezesha kufika hapa. Natafuta neno zaidi ya Asante sioni. Nashukuru sana. Asante, Asante tena na tena"..


Walter ni mkazi wa Mbeya ingawa katika mashindano haya anawakilisha jiji la Dar es salaam kwani alisailiwa akiwa huko.

Nov 8, 2012

Madam Rita: Diamond atasubiri saanaa kwa Walter Chilambo


Interview ya Stans wa Mbeya fm na Walter wa EBSS

Kwa waliokosa Interview hiyo jana mida ya saa 9 Mbeya fm sikiliza hii hapa...

PROFESSOR JAY FOUNDATION NA NISHIKE MKONO TOUR SOON KUANZA DAR

Msanii wa Bongo Fleva almaarufu kama Professor jay kwa hapa Tze anayetamba na ngoma zake kadhaa kali kama Hello,Nikusaidiaje,Kamiligado na nyinginezo kali sasa

Latest info ambayo tunayoifahamu kutoka kwa msanii huyu ni kwamba wiki iliyopita alikuwa akitoa misahada mbalimbali katika hospital ya Tumbi pamoja na mafunzo ya Elimu sasa leo amefunguka na kusema kwamba Professor Jay Foundation na Nishike mkono Tour inaendelea kwa hiyo watu wasidhani kwamba wamefanya tu maeneo ya Pwani kwani alifunguka na kusema kwamba ndiyo wapo katika mazungumzo na kamati nzima juu ya kutoa huduma za Afya na Elimu kwa hapa Dar es Salaam na akasema kwamba sehemu ambayo wamepanga kutoa huduma hizo ni maeneo ya Kigamboni siku ya tarehe 17 mwezi huu.Baada ya kusema hayo aliweza kuwa shukuru wale wote waliofika Pwani na kutoa kila ambacho wanacho.@Info by Professor jay...

Nasikia Diamond Atafunikwa tena kama ktk hii Video, Check up


Nov 7, 2012

Mbeya: Kandoro atishia Kumtimua Mkandarasi wa wa barabara kwa kiwango cha rami wilayani Mbozi

Mkuu wa mkoa wa Mbeya ABASI KANDORO akiteta mambo na wakuu wa idara wa Mbozi mara baada ya kutembea kukagua ujenzi wa barabara.

 
Mkuu wa Mkoa ABASI KANDORO akitembelea barabara hiyo na kusema kutoa agizo la kurudiwa sababu haikizi vigezo.

Jengo Kuporomoka Ghana

Jumba la ghorofa limeporoma nchini Ghana huku watu wengi wakiarifiwa kukwama kwenye vifusi.

Waokozi wanaendelea na shughuli ya kutafuta manusura ingawa taarifa zinasema kuwa watu wawili wamefariki katika tukio hilo.

Rais wa nchi hiyo, John Dramani Mahama, ameakhirisha kampeini zake za uchaguzi utakaofanyika mwezi ujao kushughulika mkasa huo.

Naibu wake Paa Kwesi Amissah-Arthur, anaratibu juhudi za uokozi kufuatia kuporomoka kwa jengo hilo mjini Achimota .

Maafisa wanasema kuwa wanaamini takriban watu hamsini walikuwa ndani ya jengo hilo wakati lilipoporomoka asubuhi ya leo.

Mamia ya waokoaji wanawatafuta manusura kwenye vifusi kukiwa na hofu ya watu wengi kanaswa.
''Nilikuwa karibu sana na jengo hilo kwa sababu nilkuwa naenda kununua kitu madukani lakini punde nikaona jengo hilo likianza kuanguka.'' alisema makaazi mmoja Ama Okyere

"Nililazimika kukimbilia usalama wangu. Ninaamini kuwa kuna watu wengi waliokwama ndani ya vifusi kwa sababu hii ni mojawapo ya maduka ambayo yanapendwa sana na watu.'' alisema Ama Okyere

Kortin kwa Kubaka Mwanafunzi

MKAZI wa Mwenge Mlalakuwa, Dar es Salaam, Salemani Ibrahimu (28), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni akikabiliwa na tuhuma za kumbaka mwanafunzi mwenye umri wa miaka 15.

Mwendesha Mashitaka, Anita Sinare, alidai mbele ya Hakimu Jackline Rugemalila kuwa, mshitakiwa alitenda kosa hilo katika nyakati tofauti Juni mwaka huu.

Hata hivyo, mshtakiwa alikana tuhuma hizo na kuachiwa kwa dhamana. Kesi itatajwa Desemba 3, mwaka huu.

Katika kesi nyingine, mkazi wa Mburahati, Iddi Salum (36) amefikishwa mahakamani hapo akikabiliwa na kosa la kumlawiti mtoto mwenye umri wa miaka 11.

Mwandesha Mashitaka, Mussa Mnuvi alidai mbele ya Hakimu Hilda Lyatuu kuwa, mshitakiwa alitenda kosa hilo Novemba 5, mwaka huu, eneo la Magomeni Mapipa, tuhuma ambazo alizikana.

Mshitakiwa amepelekwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana. Kesi itatajwa Novemba 20, mwaka huu.

LEMA: SIPENDI UBUNGE WA RUFAA

BAADA ya Mahakama Kuu ya Arusha kumvua ubunge Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema (Chadema), kiongozi huyo amesema hatakata rufaa kwa kuwa hataki kuwa mbunge wa rufaa.


Jana Jaji Mfawidhi Kanda ya Sumbawanga, Gabriel Rwakibarila, alimvua ubunge Lema katika hukumu ya kesi iliyokuwa ikimkabili ya kupinga matokeo ya uchaguzi uliompa ubunge.

Hukumu kwa Lema Jaji Rwakibarila katika hukumu hiyo, alitaja sababu kuu nane zilizomshawishi kutengua ubunge wa Lema, zikiwamo za kutoa matusi, kashfa na kejeli katika mikutano ya kampeni.

Alisema kanuni, taratibu na Sheria ya Maadili ya Uchaguzi ya Mwaka 2010, zinakataza mgombea kutoa lugha za matusi, kashfa na kejeli na Lema alifanya hivyo huku akijua kuwa ni kinyume cha sheria.

Hoja zilizotupwa Rwakibarila alisema katika hoja kumi zilizowasilishwa mahakamani na mawakili wa wanachama watatu wa CCM waliofungua kesi hiyo, Alute Mughwai na Modest Akida, alitupilia mbali hoja mbili tu.

Alizitaja kuwa ni madai kuwa Lema katika kampeni aliwataka wananchi kutochagua mgombea wa CCM, Dk. Batilda Buriani, kwa kuwa ni mkazi wa Zanzibar, hivyo hastahili kupewa ubunge Arusha Mjini.

Jaji Rwakibarila alisema hoja hiyo haina mashiko, kwa kuwa kusema Dk. Batilda ni mkazi wa Zanzibar haina maana ya kashfa.

Hoja nyingine aliyotupilia mbali ni ya udini, ambapo ilidaiwa kuwa Lema katika mikutano yake ya kampeni alisema Dk. Batilda asichaguliwe kwani anavaa kilemba ni Al Qaeda na pia atafunga Radio Safina na kujenga Msikiti .

Jaji alisema hoja hiyo nayo haina mashiko, kwani kuvaa kilemba si kuwa Al Qaeda kwani wako wanawake wengi wanavaa vilemba na pia hakukuwa na ushahidi wa kutosha kuthibitisha kuwa atafunga redio hiyo na kujenga Msikiti.

Hoja zilizombana Lema Katika moja ya hoja zilizoungwa mkono na Jaji Rwakibarila, ni pamoja na ya Lema kuthibitika kutumia kashfa, kejeli na udhalilishaji katika mikutano yake.

Kashfa hizo kwa mujibu wa Jaji Rwakibarila, ni kauli za Lema kuwa Dk. Batilda ni hawara wa mzee wa Monduli na kwamba ana mimba ya Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa.

Hoja nyingine ni kauli ya Lema katika mikutano yake akiwataka wananchi kutomchagua Dk. Batilda kwa sababu ni mwanamke, ambapo Jaji Rwakibarila aliita kauli hiyo kuwa ni ya ubaguzi wa kijinsia.

Tume iambiwe Kutokana na sababu hizo, Jaji aliamua kutengua ubunge wa Lema na kumtaka Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, George Hubert, aiarifu rasmi Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) mara moja kuhusu uamuzi huo na kumwagiza Lema alipe gharama za kesi hiyo.

Nov 6, 2012

Alichoandika Walter ktk Mitandao yake

"Nashukuru sana mtu wangu, ni Maombi na Kura zenu tuu.. Nashukuru kuingia FAINALI na nakuomba endelea na moyo huohuo kwa kunipigia kura kwa kuandika neno EBSS12 kwenda namba 15530".

Hiyo ni status aliyoiandika Walter katika ukurasa wake wa Facebook na Twitter jana baada ya kurushwa kwa show yake ya nusu fainali iliyompelekea kuingia fainali itakayofanyika Diomond Jubilee, Ijumaa ya tarehe 09/11/2012.

Pamoja na hayo Walter aliongeza kuwa anamshukuru Mungu na watanzania kwa hatua aliyofikia kwani haikuwa rahisi kihivyo.

Pia Walter ameongelea suala la yeye kuwa amnatokea Mbeya kwani ni jambo lililokuwa linachanganya watu wengi.

"Mimi ni mzaliwa wa Mbeya na naishi huko na mama yangu na wakati wa audition za EBSS nilikuwa nipo Dar katika michakato yangu na ndio sababu nikasailiwa kama mshiriki kutoka Dar".

Aliongeza, "Naomba watu wangu waendelee na moyo huo huo wa kuwa bega kwa bega na mimi na waendelee kunipigia kura kwani kura ndio kila kitu hata kama nitapendwa vip"

Walter ni mshiriki aliyeingia FAINALI pamoja na wenzake wanne, hivyo washiriki wa EBSS walio katika fainali ni Walter, Nshoma, Nsami, Wababa pamoja na Guiter gira Salma... 

Ili kumpigia kura Walter Chilambo, andika neno EBSS12 kwenda namba 15530".

WALTER CHILAMBO WA EBSS AKIIMBA NATUMAINI RMX YA BEKA, CHECK NAYO HAPA

WALTER ALIVYOMFUNIKA DIAMOND


WALTER CHILAMBO: EBSS RnB KING


MSIKILEZE WALTER BAADA YA KUINGIA 20 BORA NDANI YA EBSS 2012

WALTER: Olwayz on Ma Mind


WALTER: NIMEINGIA MJENGONI SASA


WALTER CHILAMBO SIKU YA KWANZA NDANI YA EBSS, IMESOMEKAA?