Nov 7, 2012

Kortin kwa Kubaka Mwanafunzi

MKAZI wa Mwenge Mlalakuwa, Dar es Salaam, Salemani Ibrahimu (28), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni akikabiliwa na tuhuma za kumbaka mwanafunzi mwenye umri wa miaka 15.

Mwendesha Mashitaka, Anita Sinare, alidai mbele ya Hakimu Jackline Rugemalila kuwa, mshitakiwa alitenda kosa hilo katika nyakati tofauti Juni mwaka huu.

Hata hivyo, mshtakiwa alikana tuhuma hizo na kuachiwa kwa dhamana. Kesi itatajwa Desemba 3, mwaka huu.

Katika kesi nyingine, mkazi wa Mburahati, Iddi Salum (36) amefikishwa mahakamani hapo akikabiliwa na kosa la kumlawiti mtoto mwenye umri wa miaka 11.

Mwandesha Mashitaka, Mussa Mnuvi alidai mbele ya Hakimu Hilda Lyatuu kuwa, mshitakiwa alitenda kosa hilo Novemba 5, mwaka huu, eneo la Magomeni Mapipa, tuhuma ambazo alizikana.

Mshitakiwa amepelekwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana. Kesi itatajwa Novemba 20, mwaka huu.