Waokozi wanaendelea na shughuli ya kutafuta manusura ingawa taarifa zinasema kuwa watu wawili wamefariki katika tukio hilo.
Rais wa nchi hiyo, John Dramani Mahama, ameakhirisha kampeini zake za uchaguzi utakaofanyika mwezi ujao kushughulika mkasa huo.
Naibu wake Paa Kwesi Amissah-Arthur, anaratibu juhudi za uokozi kufuatia kuporomoka kwa jengo hilo mjini Achimota .
Maafisa wanasema kuwa wanaamini takriban watu hamsini walikuwa ndani ya jengo hilo wakati lilipoporomoka asubuhi ya leo.
Mamia ya waokoaji wanawatafuta manusura kwenye vifusi kukiwa na hofu ya watu wengi kanaswa.
''Nilikuwa karibu sana na jengo hilo kwa sababu
nilkuwa naenda kununua kitu madukani lakini punde nikaona jengo hilo
likianza kuanguka.'' alisema makaazi mmoja Ama Okyere
"Nililazimika kukimbilia usalama wangu.
Ninaamini kuwa kuna watu wengi waliokwama ndani ya vifusi kwa sababu hii
ni mojawapo ya maduka ambayo yanapendwa sana na watu.'' alisema Ama
Okyere