COMEDY

Masanja Mkandamizaji:
SIKIA HII MWANAWANE: Jamaa alikosea kutuma Pesa ktk M-Pesa, Tsh. 500,000/= ikaenda namba nyingine, kuona hivyo akaumiza akili akatuma meseji ifuatayo kwenye namba ihiyo."UMETEULIWA KUINGIA CHAMA CHA FREEMASON NA UMETUMIWA PESA, BAADA YA DAKIKA 15 ATAKUFA MWANAO UMPENDAE. HARAKA KAA NJIA PANDA GARI YETU NYEUSI ITAKUFUATA UJE UNYWE DAMU YAKE.! KAMA UMESHINDWA MASHARITI RUDISHA PESA HARAKA KABLA YA MAAFA".. baada ya dakika 1 tu jamaa akaona salio limerudi, chezea mtoto wewe.

Jamaa analonga na bebee:

JAMAA.. Babie nakupenda sanaa japo MUNGU hajanijaalia pesa nyingi Kama rafiki Yangu JOHN, ambaye tumecheza naye tangu utotoni,lkn mwenzangu Ana Magari,Maduka,Hotel yaani anahela sana,ila Mimi nakupenda pamoja Na umasikini WANGU

MDADA.. JAMANII BABIEE !!! SIKIA KAMA KWELI UNANIPENDA NAOMBA NAMBA YA HUYO JOHN!!
UNGEJIBUJE MWANAWANE..


HESABU.
Mama: Mwanangu,njoo nikufundishe hesabu.
Dogo: Haya mama.
Mama: Kwa mfano shangazi yako akikupa maandazi mawili, halafu akakupa tena maandazi mawili jibu lako litakuwa nini?
Dogo: Asante shangazi..