Dec 19, 2012

MAKAMUA: KAZI YA QJ NI KUCHOMELEA

Rafiki mkubwa wa QJ ambaye pia ni msanii, Makamua, amefunguka kuhusu rafiki yake na kazi anayoifanya kwa sasa kuwa ni ya KUCHOMELEA.

Makamua akiongea “ni kweli QJ karudi kwenye hiyo kazi lakini ni sawa tu pia mi sioni kama kuna tatizo, sasa hivi anajipanga manake anataka kufungua sehemu yake yeye mwenyewe kwa sababu amekua akifanya kazi kwa watu, hata sisi tumemshauri ajiajiri mwenyewe kwa sababu ndio kitu ambacho anakipenda, sasa hivi anafanya kazi kwenye ofisi ya mtu”
Makamua na QJ kwa Stage..!
QJ alitangaza kuokoka na kuachana na bongofleva na kuthibitisha rasmi kwamba kwenye muziki wa gospel ndiko atakakosikika sasa hivi ambapo Makamua pia amesisitiza kwamba kazi kubwa anayoifanya QJ sasa hivi ni hiyo ya kuchomelea vyuma.

Kwenye mistari mingine pia Makamua amekanusha kuwa na uhusiano mbaya na staa mwenzake wa R’n'B ambae ni mshindi wa tuzo ya KTMA Ben Pol, kasema hakuna ukweli wa hizo taarifa na hata hivyo wamekua na maongezi ya kufanya single pamoja...