Wizara ya usalama ya Marekani
(Pentagon) imetishia kumpeleka mahakamani mwanajeshi alieandika kitabu
kuhusu jinsi yeye na wenzake walivyomuua gaidi Osama Bin Laden aliekua
kiongozi wa Al Qaeda.
Mwanajeshi huyo aliekua kwenye
kundi la wanajeshi wenye ujuzi wa hali ya juu alikua mtu wa pili kuingia
chumbani alipokuepo Osama ambapo kwenye kitabu alichoandika anaeleza
kwamba Osama hakua na silaha yoyote walivoingia chumbani kwake, taarifa
ambayo inatofautiana na iliyotolewa na Pentagon.
Kanuni zinazoongoza oparesheni
kama iliyomuua Osama zinawanyima wanajeshi waliohusika kutoa siri au
kutangaza chochote ndio maana anaonekana kavunja makubaliano.
Sasa hivi vyombo vya habari
vimeanza kuhusisha hicho kitabu na kampeni za urais jambo ambalo
mwanajeshi huyo amelikataa na kusisitiza kwamba amekiandika hicho kitabu
ili kuweka hadharani ukweli bila kulenga chama chochote cha siasa wala
mgombea.
Matt Bissonnette(36) ambae
hafurahii uongozi wa rais Obama, alikua hataki kutambuliwa kwenye vyombo
vya habari lakini tayari jina lake limeshajulikana na limesambaa hivyo
ilimlazimu kujificha.