Sep 7, 2012

BAADA YA KURUDI, NOKIA DON'T BREAK THE BEAT WANASEMAA,,,,,,,,


Ali aka Robin na Njama Ndio walio shine zaidi Tanzania na kwenda kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Freestlye kupitia Nokia Dont Break The Beat.Mobi.

Mshindi wa nne alitoka Tanzania nae ni Njama na wapili ni Ali aka Robin. Baada ya Njama kurudi Tanzania ametangaza kwamba anatafuta lebel au deal ya kufanya kazi na producer yoyote Tanzania atakaye ingia mkataba nae .

Pia amesema anawakubali ma producer kama Duke wa M Lab,Lamar na Tongwe Records, na Alivyokuwa kenya alikutana na Cannibal na tayari wana mpango wakufanya collabo.

Ali kwa sasa tayari amesha fanya nyimbo kadha na zipo studio  zikifanyiwa final mixing na pia amefunguka kuwa kufanya kazi na Belle 9 ni kitu anacho taka kufanya baada ya kukamilisha project zake za kwanza .