Sep 16, 2012

DITTO TUZONI

Msanii wa Bongo Fleva Lameck Ditto wa THT ametajwa katika wasanii wanao gombania Tuzo za Radio France International Discoveries kutoka Ufaransa .Kwenye hii tuzo wasanii kumi kutoka Africa huchaguliwa na kupambanishwa ,Ditto ameingizwa kwenye tuzo hizi kupitia nyimbo tofauti kama Wapo na Mi Amini na mshindi wa Tuzo hii atapata Euro Elfu kumi na mkataba wa kufanya show za live katika nchi 18 duniani.
Maeneo ya show hizi yatakuwa Afrika magaribi ,Marekani na Europe, Mkataba huu pia una kipengele cha promotion atakayo fanyiwa na Vituo vya Radio France. Nia ya Radio France kufanya Tuzo hizi ni kutangaza mziki wa Africa Duniani na mshindi wa kwanza wa tuzo hii kutoka Africa Mashariki alikuwa Maurice Kirya 2010 ,alishinda Euro 18,000 na kufanya show Mjini Paris na Tour ya Africa Ya Mwaka Mzima.