Dec 1, 2010

Wakazi Mogadishu hawawataki Al Shabaab

Matokeo ya utafiti wa kura ya maoni iliofanywa mjini Mogadishu, kwa niaba ya BBC, yamebainisha robo tatu ya wakaazi wa mji huo, hawataki wapiganaji wa kundi la Kiislamu wa Al Shabaab, kutwaa uongozi wa Somalia.
Maandamano ya kupinga kundi la Al Shabaab
Maandamano ya kupinga kundi la Al Shabaab

Uchunguzi huo umeonesha wengi wa wakaazi wa Mogadishu wanaamini kuwa kundi la Al Shabaab ni la kigaidi.
Wengi wao wahisi kundi hilo ni la upinzani. Asilimia hamsini ya wakaazi wa mji wa Mogadishu wanasema jamii ya kimataifa imelipuuza taifa lao ambalo halijawa na serikali kwa karibu miaka ishirini.
Utafiti huo umeendelea kuonesha asilimia tisini na mbili ya wakaazi wa mji huo hawana uwezo wa kukidhi mahitaji muhimu na ya kimsingi kama chakula na ulifanywa katika maeneo yanayodhibitiwa na kundi hilo la Al Shabaab.