Dec 21, 2012

LORD EYEZ: UKWELI KUHUSU MIMI, RAY C, MADAWA&WIZI.

Baada ya kimya cha muda mrefu, msanii wa Hip Hop Tanzania kutoka ktk kundi la WEUSI, LORD EYEZ, amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu habari na kila kinachoendelea kuhusu yeye.

Lord Eyez amesema kuwa ameathirika sana kutokana na taarifa zilizokuwa zinaendelea kusambaa kuhusu yeye, lakini kwa watu waliomfahamu walijua kuwa ni janga tuu na wasiomjua ilikuwa kama vile ila habari hizo sio za kweli..

Kitu kilichotokea nilipigiwa simu nikasema nilipo mara zilitokea ndinga ghafra na kuatack kwangu wakiwa na Dimpoz. Walikuwa kama watu 15 na gari zao 15 wakidai vifaa vya Ommy vimeibiwa huku wakisema kuwa mimi ndio namjua aliyemuibia huyo Dimpoz.
Msanii LORD EYEZ
Katika hayo magari matatu waliyokuwa nayo halikuwepo gari la polisi na sikukamatwa na polisi ni raia walinishikilia muda mrefu sana bila kunipeleka polisi huku kuonyesha kutoelewana hata wenyewe na jioni kunipeleka kuliona gari lililoibiwa na kukuta watu wa kupiga picha wameandaliwa.
Hapa alikuwa ktk eneo la tukio la Dimpoz kuibiwa
Amesema kuwa anajua kuwa tu ni visa, na hii ilianzia kuwa kuna mtu nilionekana nae kuwaanahusika na hilo.

Na kama ikitokea kuwa kesi imeisha na kukutwa sina hatia nitakuja kuwaambia nitakachoamua. Kwani kwa sasa siwezi kuongea mengi kwani mengi ni ushahidi na kesi inaendelea.

Pia kuhusu Ray C, Amefurahi sana na kusema kuwa Mungu kafanya miujiza yake na pia Ray C ni rafiki yangu kama mwanzo.