Baada ya siku nyingi kupita, Mh. Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi "Sugu" Aliandika jana ktk ukurasa wake wa FaceBook kuwa anatangaza vita na madactari baada ya mara zote kuwatetea bungeni kutokana na vitendo vya rushwa ktk kitengo cha mifupa Rufaa Mbeya.
|
Sugu aliandika kwa herufi kubwaa.. ""NATANGAZA VITA NA MADAKTARI: MARA ZOTE NIMEKUWA MSTARI WA MBELE KWA
KUTETEA HAKI NA MASLAHI YA MADAKTARI WETU BUNGENI,LAKINI KWA NIABA YA
WANANCHI WA MBEYA LEO NATANGAZA VITA NA MADAKTARI WA HOSPITALI YA
RUFAA-MBEYA KITENGO CHA MIFUPA,WAMENICHOSHA KWA RUSHWA AMBAYO IMEKITHIRI
KAMA AMBAVYO SIJAWAHI KUONA MAHALI POPOTE.WANANCHI
MASKINI WANALAZIMISHWA KULIPA TSHS 300,000/= MPAKA TSHS 500,000/= KWA
AJILI YA KUWEKEWA JUST A 'P.O.P', AU VINGINEVYO MGONJWA ANAAMBIWA ANA
TATIZO KUBWA LINALOHITAJI OPERESHENI NA KWAMBA AENDE PERAMIHO AU
MUHIMBILI-DAR...KUNA TAARIFA KUWA KUNA WANANCHI WENGI WAMEKUFA NA
WENGINE KUKATWA MIKONO NA MIGUUU KWA KUWA TU HAWAKUWA NA FEDHA ZA KUWAPA
MADAKTARI HAO WA RUFAA-MBEYA...SASA KWA KUWA NIMEJARIBU SANA
KUSHIRIKIANA NA SERIKALI AKIWEMO RC MH. KANDORO BILA MAFANIKIO KWA MADAI
KUWA HAKUNA USHAHIDI,SASA WAKIENDELEA KUKAA KIMYA NA WATU WETU
WANAENDELEA KUTESEKA NA KUFA BASI TUTALAZIMIKA KUTUMIA NGUVU YA UMMA
KUJITETEA KAMA KAWAIDA YETU"" |
Kiilichotokea leo ktk mahakama kuu ya Mbeya ni kuwa Daktari bingwa wa kitengo cha upasuaji akamwatwa na rushwa ya shilingi
laki moja, afikishwa mahakamani leo..
|
Daktari huyo akifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza.. |
Habari kamiliitawajia hapa baada ya kesi kumalizika hapahapa..