Dec 22, 2012

YOUR NEW MISS EAST AFRICA

Ni m'T'Zee Jocelyne Dyna Maro (22)
Walipokuwa Top 5.
Jocelyne Dyna Maro (22) Miss East Africa Tanzania ametangazwa mshindi katika shindano hilo lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam akiwashinda warembo wenzake kutoka mataifa mbalimbali ya Ukanda wa Afrika Mashariki na nchi Jirani na Ukanda huo. Jocelyne ni mchaga ameishi Uingereza, Afrika Kusini, Kenya na Ivory Coast.

Jocelyne Maro Mtanzania wa kwanza kushinda taji hilo toka lililpoanzishwa amejinyakulia zawadi zenye thmamani ya dola za kimarekani 30,000 likiwemo Gari aina ya Toyota Verossa, mara baada ya majaji kumtangaza mrembo huyo ukumbi mzima ulilipuka kwa shangwe huku watu mbalimbali wakimpongeza kwa ushindi wake.