Dec 24, 2012

MILLARD AYO: LEO MIAKA 6 NYUMA

ALICHOANDIKA MILLARD AYO KATIKA PAGE YAKE YA FACEBOOK IMENIFANYA KUFIKIRIA V2 VINGI SANA.. Kama umemfuatilia huyu jamaa, ana bonge la History ingawa huwa analitoa nusu nusu kama hivi..

HIKI ndicho alichoandika..

"Miaka 6 iliyopita wiki kama hii ndio nilipata tuzo ya kwanza ya Utangazaji kutoka Tanzania Radio Awards, nikapandishwa mshahara toka elfu tano mpaka elfu kumi kwa wiki kwenye radio niliyokua nikifanyia kazi, sikutamani kufanya kazi nyingine japo nilikua naishi kwenye hali ngumu sana, niliahidi nitapambana ili nifanikiwe kwa hii kazi kwa sababu naamini Mungu ameweka kitu ndani yangu, nasema Amen leo nina maisha ninayoridhika nayo kabisa tena sana, Namshukuru Mungu sana kwa hilo! hii ni maalum kwa watu wangu wote wa nguvu ambao wanapitia shida, hawana kazi au wanafanya kazi lakini mafanikio hawayaoni, wanatafuta kazi kila siku hawapati, ukweli ni kwamba SUBIRA ni kila kitu, Nidhamu ni kila kitu, Maombi ni kila kitu, Kujituma ni kila kitu! kutokakuta tamaa ndio muhimu kabisa."
Millard akihojiana na Rozee..
Kila la kheri kaka ktk kazi zako..