Dec 18, 2012

WEUSII FUNGA MWAKA

Fahamu kwamba baada ya rapper Lord Eyes kupata tuhuma za wizi wa vifaa vya gari la Ommy Dimpoz ni watu wengi wamekua na hamu ya kujua ataongea nini na atafanya nini kwenye siku yake ya kwanza kwenye stage toka hiyo ishu itokee.

Hajaonekana kwenye stage yoyote mpaka sasa na tayari kwenye Exclusive interview na millardayo.com alisema ana nyimbo tatu kichwani kuhusu yote yaliyotokea toka apate hizo tuhuma za wizi, na aliahidi pia kwamba december hii ndio ataachia single moja kati ya hizo.

Time imefika sasa hivi manake Weusi wanataka taarifa ikufikie kwamba stage ya Maisha Club december 23 2012 itamilikiwa na wao kwenye ‘Funga mwaka la weusi’

Kuna sababu kubwa za wao kuwa kwenye stage usiku huo, kwanza ni utambulisho wa single mpya ya Lord Eyez, ishu ya pili ni uzinduzi wa Bum Kubam DVD ya Nikki wa II ambapo G NAKO, JOH MAKINI,  NIKKI WA PILI,  BONTA na LORD EYEZ stage itawahusu kwa kadi ya mwaliko utakayoichangia elfu 10 tu.