Jan 30, 2014

Pictures: Hii ni zaidi ya Catoon, Check Out

 Click hapa chini kutizama picha zaidi...

Daah! Mwandishi mwingine wa BBC afariki dunia

Mwandishi wa BBC Ann Waithera afariki
Mwandishi wa BBC nchini Kenya Ann Waithera ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 39 baada ya kuugua Saratani kwa muda mrefu..

Gosby kufanya "SCARFACE VALENTINE'S DAY MASSACRE II" na Hiki ndicho alichokisema FB

 Gosby kufanya "SCARFACE VALENTINE'S DAY MASSACRE II" Hiki ndicho alichokisema katika ukurasa wake wa FaceBook.......
Nafanya mixtape SCARFACE VALENTINE'S DAY MASSACRE 2, unadhani rapper gani ahusike na yeye kwenye hii mixtape janangu ashushe bars..

LAMAR: Soon kuanzisha kipindi cha uhalisia wa kazi zake akiwa STUDIO na mengineee

Kwa story zaidi kuhusiana na hili tembelea Bongo5 kwa kubofya HAPA!

Steal New: Msami - Soundtrack (Official Video)

Jan 27, 2014

T was #FamilyDay ya HighlandsFM @ ManyanyaInn, Ilikuwa poa sana, checkna hizi Pics Kadhaa

 Check na pics zangu kadhaa kucheck ilivyokuwa...
Angalizo: Hii ni blog yangu binafsi, hivyo naweza kufanya lolote  nitakalo..

Jan 26, 2014

Leo katika Historia, Miaka 114 iliyopita, kutoka Iran

Siku kama ya leo miaka 114 iliyopita mfamasia wa Kijerumani Felix Hoffmann alitengeneza dawa ya kwanza ya kutuliza maumivu. Dawa hiyo hii leo inajulikana kwa jina la Aspirin. Waingereza pia waliamua kutengeneza dawa hiyo katika kipindi cha Vita vya Kwanza vya Dunia baada ya uingizaji dawa hiyo nchini Uingereza kusimamishwa. Mbali na kutuliza maumivu, Aspirin ina sifa nyingine kadhaa ambazo ni pamoja na kuzuia damu isigande na kuzuia mshtuko wa moyo.

Jan 12, 2014

Wanyaka majambazi sugu Katavi, yakiwa na bunduki za KIVITA. KIVITAAAH!!!!



JESHI la Polisi Mkoa wa Katavi linawashikilia watu 3 kwa tuhuma za kukutwa na bunduki ya kivita aina ya G3, ikiwa na risasi zake tisa wakati wakisafirisha silaha hiyo kutoka Mpanda kuelekea Tunduma, Mbeya.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, amewataja watuhumiwa  waliokamatwa kuwa ni  Simon Kasobhile, maarufu kwa jina la Kamwela mkazi wa Ileje, Mbeya. Wengine ni Bilau Rashid, maarufu kwa jina la Maftah, mkazi wa Rukwa  na Martine John mkazi wa Tunduru, waliokamatwa Januari 10, majira ya usiku katika Kitongoji cha Matandalani, Kata ya Sitalike, wilayani Mlele.
Kwa mujibu wa kamanda Kidavashari, watu hao walikamatwa  wakiwa kwenye gari aina ya Toyota  Cruiser Prado,  lenye namba za usajili T 564 ABW lililokuwa likiendeshwa na George Kiluli, mkazi wa Mpanda. Amesema  dereva wa gari hilo alikuwa anampeleka mdogo wake, Gabriel Samwel, Shule ya Sekondari Laela, Sumbawanga na alipofika eneo la City mjini Mpanda alisimamisha gari na kupakia abiria wakiwamo watuhumiwa hao.

KIFO cha Kagame, Wa2 wa Rwanda wafanya sherehe

Kwa masaa kadhaa Ijumaa nyakati za asubuhi, kulikuwa na fununu kuwa Rais wa Rwanda, Paul Kagame ameaga dunia na taarifa hizo zilienea hadi mji wa Goma Mashariki mwa Congo. Wengi walisherehekea baada ya kupata habari hizo.

MSIBA: TAJI Liundi afiwa na baba yake mzazi, R.I.P our papaa Jaji George Bakari Liundi



ATANGAZA TAARIFA LEO
TAARIFA YA MSIBA: Nasikitika kutangaza kifo cha Baba Mzazi Jaji George Bakari Liundi kilichotokea ghafla leo Jumapili saa 7 mchana. 
Msiba upo KEKO JUU KJ 60(Nyuma ya Mgulani Shule ya Msingi). 
Taratibu za mazishi zinaendelea. 
Mawasiliano: 0787 888 799.

Jan 10, 2014

Yaya Toure atwaa tuzo ya mwanasoka bora Afrika '13

Mchezaji wa kati wa timu ya soka ya Manchester City ya Uingereza, Yaya Toure, amenyakua tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Shirikisho la Soka la Afrika, CAF.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast amenyakua tuzo hiyo na kuwapiku washindani wake wawili Didier Drogba anayesakata kabumbu katika timu ya soka ya Galatasaray ya Uturuki na kiungo wa Chelsea na timu ya taifa ya Nigeria John Obi Mikel.

Hii ni mara ya tatu mfululizo kwa Yaya Toure kushinda tuzo ya mchezaji bora wa CAF, baada ya mwaka 2011 na 2012 kujinyakulia pia tuzo hiyo. Wakati huo huo kocha wa timu ya soka ya taifa ya Nigeria Stephen Keshi amenyakua tuzo ya kocha bora wa mwaka barani Afrika katika soka.

Katika sherehe za kuwatangaza waliong'ara katika soka barani Afrika mwaka 2013 huko Lagos Nigeria, Keshi alishinda tuzo ya kocha bora.

Jan 7, 2014

Historia: Siku kama ya leo miaka 690 Iliyopita

Siku kama ya leo miaka 690 alifariki dunia mtalii mashuhuri wa Kiitalia Marco Polo. Alizaliwa katika mji wa Venice nchini Italia na alianza safari iliyokuwa na mikasa mingi akiwa na umri wa miaka 18 akiwa pamoja na baba yake. Safari ya kitalii ya Polo katika nchi za Mashariki iliendelea kwa kipindi cha miaka 20.
Alirejea nchini Italia mwaka 1291 na kuandika aliyoyaona katika kitabu alichokipa jina la "Maajabu". Kitabu hicho kilipata umashuhuri mkubwa duniani na alizungumzia kwa mapana na marefu kuhusu aliyoyaona katika nchi za China, Turkemanistan, Mongolia na sehemu za kusini mashariki mwa Asia.
Siku kama ya leo miaka 372 iliyopita alifariki dunia msomi mashuhuri, mnajimu na mtaalamu wa fizikia wa Italia Galileo Galilei akiwa na umri wa miaka 78.
Alizaliwa katika mji wa Pisa na alisoma fasihi hadi alipokuwa na umri wa miaka 19 na baadaye akajishughulisha na fizikia na hisabati. Galileo alitumia lenzi iliyovumbuliwa na msomi na mnajimu mashuhuri wa Kiislamu, Ibn Haitham kutengeneza darubini ya elimu ya nujumu kwa ajili ya kutazamia nyota na sayari

Jan 5, 2014

UPDATES: MV Kilimanjaro, 5 wafa, wengine HOFU!!

WATU kadhaa wanahofiwa kupoteza maisha ikiwa 5 wathibitishwa kufa baada ya boti ya MV Kilimanjaro 2 inayomilikwa na shirika la Azam Marine kukumbwa na dhoruba katikati ya bahari, wakati ilipokuwa safarini kutoka kisiwani Pemba kuelekea kisiwani Unguja.
Baadhi ya habari nchini Tanzania zimelinukuu jeshi la polisi likidai kuwa, baadhi ya abiria waliokuwemo kwenye boti hiyo walichukua majaketi ya kujiokolea na kuyatupa nje ya boti hiyo.
Hata hivyo watu mbalimbali waliokuwemo kwenye boti hiyo walipohojiwa na vyombo vya habari wamesema kuwa majaketi yaliyokuwemo yalikuwa hayatoshi na watu waliyapata kwa kugombania.
Hadi hivi sasa idadi hasa ya watu waliopoteza maisha yao haijajulikana. Taarifa zinaongeza kuwa, boti hiyo ilikuwa na abiria 69 watu wazima, abiria watoto 60 na mabaharia wanane.
Iliondoka saa mbili asubuhi kisiwani Pemba kuelekea kisiwani Unguja, na ilipofika katika eneo la Nungwi bahari ilichafuka na boti ikaanza kuyumba.

Jan 2, 2014

LEO katika Historia, Miaka 1435 iliyopita...


Siku kama ya leo miaka 1435 iliyopita, Mtume Muhammad SAW alianza Hijra yake ya kuhama Makka na kuelekea Madina, ikiwa imepita miaka 13 tokea alipobaathiwa na kupewa Utume. Mtume wa Allah alihajiri Makka kutokana na kushadidi vitimbi vya washirikina wa mji huo ambao walikusudia kumdhuru na kumuua wakati wa usiku akiwa amelala nyumbani kwake. Imam Ali AS alijitolea mhanga, kwa kuamua kulala kwenye kitanda cha Mtume, ili maadui wasitambue kwamba Mtume wa Allah tayari ameshaondoka mjini Makka. Inafaa kuashiria hapa kuwa, tukio la kuhajiri Mtume SAW lilikuwa ni mwanzo wa kalenda ya Kiislamu, kwani barua zote zilizokuwa zikipelekwa kwa wakuu wa makabila na shakhsia maarufu zilikuwa zikiandikwa kwa kufuata kalenda hiyo.Siku kama ya leo miaka 1370 inayosadifiana na tarehe Mosi Rabiul Awwal mwaka 65 Hijria, ilianza harakati ya Tawwabin kwa lengo la kulipiza kisasi cha kuuawa shahidi Imam Hussein AS pamoja na wafuasi wake watiifu. Awali, watu wa Kufa walimuomba Imam Hussein AS aelekee mjini humo kwa lengo la kuongoza harakati dhidi ya utawala wa kidhalimu wa Yazid bin Muawiya. Tawwabin ni kundi la watu wa Kufa ambalo lilijuta kwa kushindwa kutekeleza ahadi zake na kumuacha Imam Hussein na wafuasi wake wachache peke yao wapambane na majeshi ya Yazid. Kwa minajili hiyo watu hao walitubia makosa yao na kuamua kuanzisha harakati ya kulipiza kisasi wakiongozwa na Suleiman bin Sorad dhidi ya jeshi la Yazid.

Siku kama ya leo miaka 21 iliyopita, inayosadifiana na tarehe 3 Januri 1993, yalitiwa saini  makubaliano ya kupunguza silaha za atomiki kati ya Boris Yeltsin, Rais wa zamani wa Russia na George Bush 'baba', Rais wa zamani wa Marekani. Kwa mujibu wa makubaliano hayo, nchi hizo mbili zilipaswa kupunguza theluthi mbili za silaha zao za atomiki. Hata hivyo, mnamo mwezi Aprili mwaka 2010 Russsia na Marekani zilitiliana saini makubaliano mapya ya START ambayo yalikuwa na lengo la kupunguza vichwa vya makombora 1,550 ya nyuklia.
Na siku kama ya leo miaka 25 iliyopita, inayosadifiana na tarehe 13 Dei 1367 Hijria Shamsia, Imam Khomeini (MA) Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu alimtumia ujumbe Mikhail Gorbachev, Rais wa mwisho wa Urusi ya zamani akimtaka  asilimu na kuachana na fikra za Kimaksi. Ujumbe huo wa Imam Khomeini MA ulipelekwa na Ayatullah Jawad Amoli, mmoja wa maulama wakubwa hapa nchini.