JESHI
la Polisi Mkoa wa Katavi linawashikilia watu 3 kwa tuhuma za kukutwa na bunduki
ya kivita aina ya G3, ikiwa na risasi zake tisa wakati wakisafirisha silaha
hiyo kutoka Mpanda kuelekea Tunduma, Mbeya.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, amewataja watuhumiwa waliokamatwa kuwa
ni Simon Kasobhile, maarufu kwa jina la Kamwela mkazi wa Ileje, Mbeya. Wengine
ni Bilau Rashid, maarufu kwa jina la Maftah, mkazi wa Rukwa na
Martine John mkazi wa Tunduru, waliokamatwa Januari 10, majira ya usiku katika
Kitongoji cha Matandalani, Kata ya Sitalike, wilayani Mlele.
Kwa
mujibu wa kamanda Kidavashari, watu hao walikamatwa wakiwa kwenye gari
aina ya Toyota Cruiser Prado, lenye namba za usajili T 564 ABW
lililokuwa likiendeshwa na George Kiluli, mkazi wa Mpanda. Amesema
dereva wa gari hilo alikuwa anampeleka mdogo wake, Gabriel Samwel, Shule ya
Sekondari Laela, Sumbawanga na alipofika eneo la City mjini Mpanda alisimamisha
gari na kupakia abiria wakiwamo watuhumiwa hao.