Sep 16, 2012
DITTO TUZONI
Msanii
wa Bongo Fleva Lameck Ditto wa THT ametajwa katika wasanii wanao
gombania Tuzo za Radio France International Discoveries kutoka Ufaransa
.Kwenye hii tuzo wasanii kumi kutoka Africa huchaguliwa na kupambanishwa
,Ditto ameingizwa kwenye tuzo hizi kupitia nyimbo tofauti kama Wapo na
Mi Amini na mshindi wa Tuzo hii atapata Euro Elfu kumi na mkataba wa
kufanya show za live katika nchi 18 duniani.
Maeneo ya show hizi yatakuwa Afrika magaribi ,Marekani na Europe, Mkataba huu pia una kipengele cha promotion atakayo fanyiwa na Vituo vya Radio France. Nia ya Radio France kufanya Tuzo hizi ni kutangaza mziki wa Africa Duniani na mshindi wa kwanza wa tuzo hii kutoka Africa Mashariki alikuwa Maurice Kirya 2010 ,alishinda Euro 18,000 na kufanya show Mjini Paris na Tour ya Africa Ya Mwaka Mzima.
Maeneo ya show hizi yatakuwa Afrika magaribi ,Marekani na Europe, Mkataba huu pia una kipengele cha promotion atakayo fanyiwa na Vituo vya Radio France. Nia ya Radio France kufanya Tuzo hizi ni kutangaza mziki wa Africa Duniani na mshindi wa kwanza wa tuzo hii kutoka Africa Mashariki alikuwa Maurice Kirya 2010 ,alishinda Euro 18,000 na kufanya show Mjini Paris na Tour ya Africa Ya Mwaka Mzima.
Sep 10, 2012
UZINDUZI WA VIDEO YA BAADAE YA OMMY DIMPOZ NDANI YA MAISHA CLUB
Usiku wa kuamkia leo msanii anayeshikilia tuzo mbili za Kilimanjaro Ommy
Dimpozi alikuwa akizindua video yake mpya inayokwenda kwa jina la
BAADAE ambayo location zake zilichukuliwa Joz South Africa na video
kuzinduliwa Bongo ndani ya New Maisha Club kiwanja cha nyumbani.
Wasanii wenzake
walikuwepo kumsindikiza Ommy Dimpozi, msanii kama Chege Chigunda alikuwa
mmoja kati ya wasanii waliofanya poa sana na kupata shangwe nyingi
hadi kufikia time ya Ommy mwenyewe kupanda katika steji ya Maisha Club
Sep 7, 2012
BAADA YA KURUDI, NOKIA DON'T BREAK THE BEAT WANASEMAA,,,,,,,,
Ali aka
Robin na Njama Ndio walio shine zaidi Tanzania na kwenda kuiwakilisha Tanzania
katika mashindano ya Freestlye kupitia Nokia Dont Break The Beat.Mobi.
Mshindi wa
nne alitoka Tanzania nae ni Njama na wapili ni Ali aka Robin. Baada ya Njama
kurudi Tanzania ametangaza kwamba anatafuta lebel au deal ya kufanya kazi na
producer yoyote Tanzania atakaye ingia mkataba nae .
Pia amesema
anawakubali ma producer kama Duke wa M Lab,Lamar na Tongwe Records, na Alivyokuwa
kenya alikutana na Cannibal na tayari wana mpango wakufanya collabo.
Ali kwa sasa tayari amesha fanya nyimbo kadha na zipo studio zikifanyiwa final mixing na pia amefunguka kuwa kufanya kazi na Belle 9 ni kitu anacho taka kufanya baada ya kukamilisha project zake za kwanza .
Ali kwa sasa tayari amesha fanya nyimbo kadha na zipo studio zikifanyiwa final mixing na pia amefunguka kuwa kufanya kazi na Belle 9 ni kitu anacho taka kufanya baada ya kukamilisha project zake za kwanza .
HUYU NDIO MWANAJESHI ALIYEANDIKA KITABU KUHUSU OSAMA
Wizara ya usalama ya Marekani
(Pentagon) imetishia kumpeleka mahakamani mwanajeshi alieandika kitabu
kuhusu jinsi yeye na wenzake walivyomuua gaidi Osama Bin Laden aliekua
kiongozi wa Al Qaeda.
Mwanajeshi huyo aliekua kwenye
kundi la wanajeshi wenye ujuzi wa hali ya juu alikua mtu wa pili kuingia
chumbani alipokuepo Osama ambapo kwenye kitabu alichoandika anaeleza
kwamba Osama hakua na silaha yoyote walivoingia chumbani kwake, taarifa
ambayo inatofautiana na iliyotolewa na Pentagon.
Kanuni zinazoongoza oparesheni
kama iliyomuua Osama zinawanyima wanajeshi waliohusika kutoa siri au
kutangaza chochote ndio maana anaonekana kavunja makubaliano.
Sasa hivi vyombo vya habari
vimeanza kuhusisha hicho kitabu na kampeni za urais jambo ambalo
mwanajeshi huyo amelikataa na kusisitiza kwamba amekiandika hicho kitabu
ili kuweka hadharani ukweli bila kulenga chama chochote cha siasa wala
mgombea.
Matt Bissonnette(36) ambae
hafurahii uongozi wa rais Obama, alikua hataki kutambuliwa kwenye vyombo
vya habari lakini tayari jina lake limeshajulikana na limesambaa hivyo
ilimlazimu kujificha.
Sep 6, 2012
FUNDI SAMWELI KUSEPA BONGO, HARUDI TENA
Yule Producer mkali kutoka pande za Kibaha Fundi Samweli amenitumia msm iliyokuwa inasema hivi
"Mpendwa mteja nitaondoka Tanzania mwezi wa 10. Sitorudi tena nitamwacha
Producer wangu Zidady studioni, ataendeleza kazi yangu namba yake ni
0719 868085
Fundi Samweli"
BAGHDAD KUENDESHWA, APEWA RATIBA YA KUISHI
Pray god kweka almaarufu kama Baghdad amesimamishwa kwa
kipindi kisichojulikana kufanya baadhi ya mambo. Kauli hii imetoka kwenye
management ambayo inamshikilia msanii huyo ambae hivi karibuni9 tuu tulisikia
amepata shavu la kuwa chini ya studio kubwa nchini marekani chofacho rec
amezuiliwa kufanya show, collabo,intaview,movie,N.k na kupangiwa rasmi ratiba
yake ya kila siku italkayomfanya yeye kufanya kazi iliyokusudiwa na mangment.
Daudi lucas alieleza ya kuwa Baghdad ametumiwa ratiba ndefu saana ya kurecord
nyimbo zake ukiangalia anatakiwa atunge ngoma kuanzia 5 mpaka 12 kwa kipindi
hichi kifupi video zaidi ya tatu kabla mwaka huu haujaisha, na kama unavyojua
aliwahi kuuguwa ugonjwa wa kisukari mazoezi anayotakiwa ni mazito saana na
jaaana tuuu tulikuwa dragon kwa ajili ya kumtafutia pumzi kwa njia ya kuogelea
na kumbe cha kushangaza alikuwa hajui hata kuogelea sooo tunajitahidi
kukimbizana na muda na kuziba baadhi ya mapungufu ya Baghdad na hata choka
nadhani unakumbuka siku niliomleta kuja kushot pamoja we can alikuwa hawezi
kutembea vizuri kwa sasa amebakiza asilkimia chache saana ili kurudi mwendo
wake wa zamani sooo tukagundua tunahitajika kumuweka mbali na club, show,
colabo, hata intaview ili asifikirie kitu kingine zaidi ya kujiandaaa kwa kuwa
intanational artist” baada ya kuyasema hayo niuliamua kumuuliza vipi kuhusu
vipindi vyake vya tv? Daudi lucas “ratiba tuliyompa huwa anapata masaa 8 ya
kupumzika 4 ya kufanya kazi na sikku za week end huwa tumempa ruhusa ya
kuchukua usafiri na kwenda kutembea na girlfriend wake nay eye alituomba ya
kuwa ana vipindi vyake anavyohitaji kuvishoot well tulimuelewa kwa kuwa
tunapenda afanikiwae na we happy all the tym tukamwambia apange sikui
atakayokuwa anashoot kisha atuambie nini anahitaji we will do it for him sooo
ni yeye kutumia muda wake wa ziada badala ya kuutumia saana kuwa na mwenzi wake
anaweza kujiiba kwa muda hata wa siku moja kati ya 2 tulizompa kuwa free tangu
asubuhi mapka jioni na kizuri kutoka kwa mpenzi wake sio mbish anamulewa saaana
Baghdad na anapenda kumsikiliza so hilo halitakuwa na matatizo nadhani na
haliingiliani kabisa na utaratibnu wake wa ki mziki” niliomba kuwa wa mwisho
kumuhioji Baghdad na nilipewa ruhusa ya kumuhoji na naamini mimi ndie nitakuwa
wa mwisho kumuhoji kwa sasa nilimuuliza Baghdad anaonaje kuwa under mangment.
baghdad“ unajua ilikuwa ni ngumu saana mi kuwa na management ingawa nyingi tuu
ziliwahi kunihitaji ila nilichokuwa nakikataa huku hakipo, so najisikia poa
sana kuwa chini ya management. 2.
Umepokeaje kali ya kusimamishwa kufanya
baadhi ya vitu “ mwanzo niliona wananizogoa ila uwezi amini kwa sasa najiona
mpya kwa kuwa sina stress yoyote zaidi ya kutunga tuuuu! 3. Una lolote kwa kuwa
hatutaongea tena kwa muda usiojulikana “ daaa watu wangu wasinie,lewe vibaya
watangazaji watakaoniita kwenye intaview nikikataa wasinbielewe vibaya, wadau
wa mziki nia ya kufanya hivi ni kuandaa kitu kizurio so nawaombeni kwa lolote
msiache kuniambia na mimi nitalifikisha kwenye mangment yangu page yangu ya
mwanzo fb imejaa so wanicheki kwenye pag mpya Baghdad pg wasiweke kweka
waniambie lolote ila kwa intaview, collabo wapige kwenye 0716 89 00 85
wataongea na management. Stop…………….
Kufanya intaviews, colabo, shows, movie, hata kunaniliu na naniliu wake nayo
stoooop Baghdad ekheee nakutakia ,mafunzo mema ya kuogelea ukishajua niambie
tushindane!
IZZO B: NIPO KIBIASHARA, MBEYA ALL STAR SIHUSIKI
Rapper Izzo Buzness
amefunguka kuhusu Mbeya Allstars na kusema hakujua kuhusu hio nyimbo wala imetengenezwa
wapi na hajahusishwa.
Izzo amesema kuwa hajakataa
kufanya Mbeya All Stars ila kwa sasa huu mziki ni biashara na kila unachifanya
uwe na malengo sio ku copy na ku paste tu.
“Kigoma All Stars wamefanya
kitu kizuri na wame safiri kwenda Kigoma na Wamefanya show, Pia wameboresha
mambo yao tofauti kupitia udhamini wa hio nyimbo, Wakati unafanya Project kama
hizi lazima ujue lengo lako na sio kufanya tu….”
Izzo alisema Tayari watu wa
Mbeya wanajua anachofanya na anawakilisha vizuri kabisa na hilo ni tosha kabisa
kwa mji wake…
“Sio sababu wao wamefanya na
sisi tufanye ila kuna mambo ya muhimu zaidi ya kufanya mziki.”
MANECK: SINA BIFU NA MARCO CHALI
Producer Maneck ambae ni
mshindi wa tuzo kwenye KTMA 2012 ameamua kuzungumza ya moyoni kwa
kuijibu kauli Dogo Janja aliyoitoa kwamba Producer huyo kauponda uwezo
wa Marco Chali.
Ishu ilianza wakiwa club Maisha
Dar es salaam jumapili iliyopita ambapo Dogo Janja anadai alikwenda
sehemu ya V.I.P na kumsalimia Maneck ambae hakujibu salamu ila
aliporomosha matusi mazito kwa Dogo Janja pamoja na kumpiga biti kwamba
asimsogelee.
Baada ya hapo Dogo Janja
akashuka chini kwenda kumwita meneja wake wa WATANASHATI ambae ni Ustaz
Juma ambapo kwa maelezo ya Dogo Janja, Maneck alianza kuiponda single
mpya ya Dogo Janja na PNC waliyoirekodi kwa Marco Chali ambayo mwanzoni
ilikua irekodiwe kwa Maneck alieiponda kwa kusema ni ya kawaida sana kwa
sababu imefanywa na Marco Chali.
Jibu alilolitoa Maneck baada ya
kusikia kwamba Dogo Janja amenukuliwa kwa hayo maneno, namkariri
akisema “ndio ninavyokwambia sitakagi watu masnich kama huyo, Marco
Chali ni mtu ambae namfil sana anafanya kazi nzuri, siwezi kuongea kitu
kibaya kwa Marco kwa sababu leo na kesho nitamfata nitamuomba msaada wa
kitu chochote kile hata material sasa nitawezaji kusema hivyo kwa mfano
sasa, Dogo Janja ni mtu ambae anataka tu kufanyaga vitu watu wapishane
kauli mambo ya kijinga ni utoto akikua nadhani ataacha hizo tabia zake,
na ndio maana nikamwambia kaa mbali sitaki uongee na mimi that’s all”
Sep 4, 2012
UGOMVI MANECK, TUNDA NA DOGO JANJA
Maelezo ya Dogo Janja
yanaamplfy kwamba juzi (September 2) walivyokua Club Maisha aliperform
akiwa na furaha kutokana na mashabiki zake waliojitokeza na alipomaliza
kuperform alishuka kwenye stage akiwa na furaha baada ya kufanya vizuri
lakini hiyo furaha ilikatishwa baada ya kwenda juu sehemu ya V.I.P.
Janja anasema alipopanda V.I.P
kumsalimia Producer Maneck alimjibu kwa dharau na kumwambia haongei na
Masnich hivyo Dogo Janja akaondoka lakini muda mfupi baadae alirudi na
kukuta Tunda Man yuko karibu na alipokaa Maneck, Janja pamoja na Tunda
walimsogelea producer huyo ambae alianza kumtukana matusi mazito Dogo
Janja.
Baada ya hapo ilibidi Dogo
Janja kushuka chini na kwenda kumchukua Ustaz Juma ambae ndio boss wa
kundi alilopo sasa Dogo Janja la Watanashati, walipofika alipo Maneck..
alianza kuiponda single mpya ya Dogo Janja aliyorekodi na producer Marco
Chali kwa kusema wimbo huo ambao mwanzo ulikua urekodiwe kwa Maneck ni
wa kawaida sana.
Kwenye line nyingine namkariri
Dogo Janja akisema “nikawa nimepanic sana sasa leo nakuja kupokea simu
eti Tunda man nae anasema nifute chorus ya ‘Anajua’ kwenye wimbo wangu,
Bro ule wimbo nimeurekodi nikiwa Tip Top na nimeifanyia show nyingi sana
Tanzania ambazo zimewaingizia hela nyingi sana, hawana ubinadamu yani
wanaponiambia mimi nifute chorus, Tunda kawafanyia watoto wangapi
chorus? Shetta, Pasha lakini mbona hamwaambii Pasha afute au labda
sababu mi mdogo, hili swala nawaachia watanzania kwa sababu ile ni haki
yangu, nilimshirikisha Tunda.. ule wimbo sio wa Tunda siwezi kufuta
chorus”
Baada ya hayo maelezo ya Dogo
Janja, Producer Maneck amezungumza exclusive na millardayo.com na
namkariri akisema “Dogo Janja alikuja akanisalimia nikamwambia ebwana
eeeh kaa mbali na mimi sihitaji kuongea na wewe kwa sababu unatabia za
kisnich sana, kuna vitu flani alivifanya siku kadhaa zimepita na
sikupendezwa navyo.. tuliandaa show ya Tunda Man pale Maisha Club
tukamwambia na akakubali kufanya na tukatangaza kwamba atakuepo sasa
mwisho wa siku akabroadcast msg kwenye BBM alafu sisi hakututumia ile
msg ila akabroadcast kwa watu kwamba hao ni matapeli, hapohapo nachat
nae namuuliza mbona umezingua anasema mi naona aibu sijui hata sura
yangu sijui nitaiweka wapi kwa bwana Captain, huku anasema hivi huku
anafanya hivi”
Tunda Man nae ametoa sababu za
kumwambia Dogo Janja afute sauti yake kwenye kolabo waliyofanya ya
‘Anajua’ na nina mkariri akisema ” sikuzungumza kwa ubaya, nimezungumza
kwa nia nzuri tu.. kwenye chorus inasema niko na Captain Tunda man alafu
mimi siko pale mashabiki wanakua kama hawakuelewi vizuri, kuna mistari
mingine inasema narun city nikiwa na JCB, narun Dar City nikiwa na T.I.P
sasa ujue kwenye show kuimba vitu kama hivyo wakati hayupo na Tip Top
vinakua havileti maana, ni kama maoni tu nimemuomba aimbie beat kwa
sababu anaweza kurekebisha ile mistari, mfano kusema narun city nikiwa
na Watanashati, kwenye show ndio abadilishe lakini kwenye audio ni sawa
ikibaki na vionjo vya mwanzo”
WALTER ASHUKURU MUNGU KUPENYA EBSS
Msanii wa kizazi kipya mkoa wa Mbeya, Eric aliyefahamika kwa jina la SpeechWise ambaye jina lake la kwenye cheti ni Walter Chilambo, ameanza safari mpya ya muziki baada ya kupenya kuingia katika 50 bora za washiriki wa EBSS kutoka katika mikoa mbalimbali Tanzania nzima.
Amezungumza na abbynm5.blogspot.com baada ya kile alichoandika katika FaceBook kuwa anamshukuru Mungu kufikia hatua hiyo kwani kwa idadi ya watu waliohudhuria Coco na vipaji vilivyokuwepo na kupenya katika 50 bora.
Pia Walter amesema kuwa kwa uweza wa Mungu anatarajia kufika mbali sana katika mashindano hayo ikiwa ni pamoja na kuifikia na kuikwapua zawadi ya mashindano hayo ambayo ni fedha za kitanzania Shilingi 50,000,000/=.
Katika status hiyo, Walter alisema "Kwa nyomi lile la Coco beach hadi kuingia 50 bora kukutana na wengine kutoka mikoani ni bonge la hatua.. Au sio wangu......" na watu kibao walimpongeza kwa hatua aliyofikia..
Pipo walivyokuwa Coco.
KILA KILA LA KHERI KATIKA HILO WALTER.
Sep 3, 2012
WAANDISHI MBEYA WALAANI MAUAJI YA MWANGOSI
WAANDISHI na Wanachi mkoani Mbeya
wamelaani vikali Mauaji ya Mwandishi wa habari wa Iringa Daudi Mwangosi, aliyeuwawa Janai katika vurugu zilizotokea
katika kijiji cha Nyororo mkoani humo.
Marehemu Mwangosi ambaye alikuwa ni Mwenyekiti wa Klabu yawaandishi wa habari mkoa wa Iringa pia alikuwa akifanya kazi katika kituo cha Chanel Ten aliuawa wakati akiripoti vurugu zilizotokea kijijini hapo baina ya Chadema na Polisi.
Marehemu Mwangosi ambaye alikuwa ni Mwenyekiti wa Klabu yawaandishi wa habari mkoa wa Iringa pia alikuwa akifanya kazi katika kituo cha Chanel Ten aliuawa wakati akiripoti vurugu zilizotokea kijijini hapo baina ya Chadema na Polisi.
IZZO-B VIDEO SOON, MBEYA ALL STAR WATISHA
Izzo
Bizness msanii wa hip hop kutoka Mbeya, baada ya kuachia video ya MWAKA
JANA sasa yuko tayari kabisa kuachia video nyingine ambayo imebeba jina
la UTARUDISHWA ambapo ndani ya wimbo huo amemshirikisha msanii kutoka
Morogoro
Belle 9.
Video hii imetengenezwa na yule yule Director ambaye alifanya video ya mwaka jana anajulikana kwa jina la Nick Dizzo kutoka E-Media.
Wakati huo huo, wasanii kutoka Mbeya (Mbeya all star) wameachia bonge la video likisifia Green city ambayo imetengenezwa na Mashada inc, production kutoka Mbeya..
Kuangalia video ya Mbeya all star tembelea blog ya DJ Choka...................
Belle 9.
Video hii imetengenezwa na yule yule Director ambaye alifanya video ya mwaka jana anajulikana kwa jina la Nick Dizzo kutoka E-Media.
Wakati huo huo, wasanii kutoka Mbeya (Mbeya all star) wameachia bonge la video likisifia Green city ambayo imetengenezwa na Mashada inc, production kutoka Mbeya..
Kuangalia video ya Mbeya all star tembelea blog ya DJ Choka...................
PICHA ZA MWANDISHI ALIYEUAWA NA POLISI IRINGA
Inaonesha Polisi walishajipanga, si unaonaaa hapo juu..
Mwili wa Marehemu Daudi ukiwa chini baada ya kulipukiwa na bomu.
Sep 2, 2012
MARLAW AONGEA KUHUSU KUTOMPA MIMBA BESTA
Katika gazeti kubwa la burudani
Tanzania la Baabkubwa lililotoka hivi karibuni ambalo husomwa na wabongo
wengi wanaopenda stori za burudani kiliandikwa kichwa cha habari kwamba
Marlaw ameshindwa kabisa kumpa mimba mkewe Besta ambae ni msanii pia.
Marlaw hapa amesema maneno 99 tu! Eti,,, “Swala la mimi kumpatia mimba mke wangu au uzao wa familia yangu ni swala langu binafsi, sidhani kama ni swala la Baabkubwa, mi sijapenda alafu na dizaini walivyoelezea yani ile interview mimi ninavyozungumza yale sio maneno yangu...........kama walinipigia simu basi ningependa kama wangeandika kile hasa ambacho hasa mimi nimekisema, nakumbuka walishawahi kunipigia simu lakini tukazungumza lakini mazungumzo hayakua vile jinsi ilivyokuja kuandikwa, yamebadilishwa.....sitochukua hatua yoyote nataka tu wanipigie simu waniambie samahani, mtu ataenipigia simu anipigie tu tumalize tuongee tu yaishe, kama wangependa kuandika kwenye gazeti lijalo waandike kile nilikiongea”
Baada ya hayo nilipochek na Baabkubwa walikua kwenye kikao lakini wakasema time ikifika msemaji atazungumza...
Marlaw hapa amesema maneno 99 tu! Eti,,, “Swala la mimi kumpatia mimba mke wangu au uzao wa familia yangu ni swala langu binafsi, sidhani kama ni swala la Baabkubwa, mi sijapenda alafu na dizaini walivyoelezea yani ile interview mimi ninavyozungumza yale sio maneno yangu...........kama walinipigia simu basi ningependa kama wangeandika kile hasa ambacho hasa mimi nimekisema, nakumbuka walishawahi kunipigia simu lakini tukazungumza lakini mazungumzo hayakua vile jinsi ilivyokuja kuandikwa, yamebadilishwa.....sitochukua hatua yoyote nataka tu wanipigie simu waniambie samahani, mtu ataenipigia simu anipigie tu tumalize tuongee tu yaishe, kama wangependa kuandika kwenye gazeti lijalo waandike kile nilikiongea”
Baada ya hayo nilipochek na Baabkubwa walikua kwenye kikao lakini wakasema time ikifika msemaji atazungumza...
Subscribe to:
Posts (Atom)