Jun 19, 2017

Jitibu kwa kutumia MAJI tu!

Mambo ya kuzingatia kabla ya kuanza tiba kwa kutumia maji:
Ifuatayo ni kanuni ya jumla ya namna ya kuyatumia maji ya kunywa katika kujikinga na kujitibu na maradhi au magonjwa mbalimbali mwilini. Kwa sababu ili maji yawe ni dawa basi kuna kanuni ya kuyanywa maji hayo.

Kanuni ya kimakisio kwa mahitaji ya maji ni; kunywa nusu ya uzito wako katika aunsi (ounces) ugawe mara mfululizo utakaoufuata kwa siku nzima. Kiasi kidogo chini au juu ya hiki, kinakubalika. Aunsi 1 = miligramu 31.25.

Kanuni ya kimakisio kwa mahitaji ya chumvi ni, Robo tatu gramu za chumvi kwa kila nusu lita ya maji, nusu kijiko cha chakula kwa kila nusu galoni ya maji au kijiko kimoja cha chakula kwa kila galoni moja la maji.

Pengine umeshageuza kichwa na kujisemea, “Wewe ni kichaa…..hicho ni kiasi kingi sana cha maji”.

Ukweli ni kuwa, ni rahisi kunywa hivyo hasa tukitumia sentensi, glasi 8 za maji zikigawanywa mara nane kwa siku (glasi 1 = ml 250 au robo lita).
Mfano, kwa mtu mwenye uzito wa kilogramu 75:


  • Badili kilogramu kwenda aunsi kwa kuzidisha mara 2.2. Hivyo, 75×2.2 = aunsi 165.
  • Tafuta nusu ya aunsi kwa kugawa aunsi na 2. Hivyo, aunsi 165/2 = aunsi 82.5.
  • Gawanya mara mfululizo utakaoamua kuufuata kwa siku nzima, mfano mara 8 kwa siku. Kwa hiyo aunsi 82.5/8 = aunsi 10.3.
  • Badili aunsi kuwa miligramu za maji. Aunsi 1 = miligramu 31.25. Kwa hiyo aunsi 10.3×31.25 = miligramu 322.

Kwa hiyo itampasa mtu huyo mwenye uzito kilo 75, kunywa ml 322 za maji mara nane kwa siku.

Namna anavyopaswa kufuata hiyo ratiba mara 8 kwa siku:
1) Akiamka tu (mfano saa 12 kamili asubuhi), cha kwanza atakunywa maji ml 322. ataendelea na shughuli zake za asubuhi

2) Nusu saa kabla ya chakula cha asubuhi (yaani saa 12:30 asubuhi), atakunywa maji ml 322. atasubiri nusu saa ipite ndipo atapata chakula chake cha asubuhi (itakuwa saa 1 kamili asubuhi).

3) Kisha kula chakula cha asubuhi, atahesabu masaa 2 na nusu ndipo atakunywa tena maji ml 322 (itakuwa saa 3 na nusu asubuhi).

4) Atahesabu masaa 2 tena ndipo atakunywa tena ml 322 nusu saa kabla ya chakula cha mchana (itakuwa saa 6 mchana) kwa hiyo nusu saa baadaye atakula chakula cha mchana (yaani saa 6 na nusu mchana).

5) Atahesabu yapite masaa 2 na nusu baada ya chakula cha mchana ndipo atakunywa tena maji ml 322 (itakuwa saa 9 kamili alasiri).

6) Atahesabu masaa 2 na nusu yapite ndipo atakunywa maji ml 322 nusu saa kabla ya chakula cha jioni (itakuwa saa 11 na nusu jioni). Nusu saa baadaye atakula chakula cha jioni (itakuwa saa 12 kamili jioni).

7) Kisha kula chakula cha jioni, atahesabu masaa 2 na nusu tena ndipo atakunywa tena maji ml 322 (itakuwa saa 2 na nusu usiku).

Muda wowote atakapokwenda kulala kuanzia saa 4 usiku atakunywa tena maji ml 322 kumalizia mara 8 zake kwa siku.

Huyo alikuwa na kilo 75, sasa na wewe andika uzito wako na utumie fomula hiyo hapo juu ujuwe ni kiasi gani cha maji unahitaji kwa siku na kisha ufuate mara hizo 8 kama zilivyopendekezwa hapo juu. Kwa staili hii ndipo maji huwa ni zaidi ya dawa.

Kila mmoja wetu sasa anaweza kutumia uzito wake kwa kutumia fomula hii na kujua ni kiasi gani cha maji anahitaji kwa siku.

Kumbuka, Kunywa maji nusu ya uzito wako katika aunsi ni kiasi cha chini kabisa, lakini mahala pazuri pa kuanzia, ikiwa ni mtu unayejishughurisha zaidi na mazoezi au unaishi katika mazingira ya joto zaidi, utahitaji zaidi ya hapo.

Sasa, hutakubali kuwa kunywa maji kwa protokolo hii ni kazi rahisi?.
Ikiwa haunywi kiasi hiki cha maji kwa sasa, unapaswa kuanza kuongeza kiasi cha ziada kwa taratibu sana. Hii itaupa nafasi mwili kujirekebisha kuendana na kiasi ulichoanza kukiongeza, na ikiwa hautaupa mwili muda wa kujirekebisha, basi maji yatakuwa kama dawa ya kukojosha (diuretic), yakisukuma madini na vitamini za mhimu nje ya mwili, pengine na kukusababishia madhara zaidi kuliko faida.

Watu wazee na watoto wadogo wanatakiwa kuanza kuongeza maji kufikia mahitaji yao kwa taratibu zaidi.

Kwa kutumia mfano wa uzito hapo juu, itakupasa kuanza na glasi 3 siku ya kwanza huku ukiongeza glasi moja zaidi kila siku inayofuata mpaka ufikie glasi zote 8.

Kumbuka kuwa, kunywa maji nusu ya uzito wako katika aunsi na kula chumvi robo tatu gramu kwa kila nusu lita ya maji, ni kanuni ya kimakisio tu. Baadhi ya wengine watahitaji maji zaidi wakati wengine watahitaji chumvi zaidi. Baada ya muda, mahitaji ya mwili kwa maji na chumvi yanaweza kuongezeka kidogo zaidi sababu ya mazingira ya joto, mazingira ya baridi au mazoezi ya viungo.

Kila mmoja lazima apate kujua kiasi cha mahitaji ya mwili wake kwa maji kuanzia sasa.

Kamwe usinywe zaidi ya aunsi 33.8 (lita moja) za maji kwa wakati mmoja ukiwa umekaa au umesimama.

Watoto wadogo kuanzia miaka 2 mpaka 12, hasa wale wepesi kujishughulisha na mazoezi wanahitaji asilimia 75 mpaka 100 za aunsi za maji katika uzito wao kwa sababu miili yao inakua muda wote na kila seli katika miili yao inayokua inayahitaji maji haya ya ziada (mytosis).

Tiba hii ya maji haitumiki kwa watoto chini ya miaka 2.

Chumvi ya kawaida ya mezani iliyoongezwa madini ya iodini, itakusaidia kidogo, chumvi ya mawe ya baharini ambayo haijasafishwa (unrefined sea salt) ndiyo nzuri zaidi sababu ya madini mengine mengi ya ziada zaidi ya 80 yaliyomo ndani yake. Chumvi ya baharini pia huwa na radha nzuri, nyeupe na umajimaji kidogo.

Namna bora za kula chumvi:
Njia ya kwanza ni kuiweka chumvi katika sehemu ya mbele ya ulimi, hakikisha unaihisi radha yake, na kisha kunywa maji juu yake yakiisafisha kuelekea chini.

Unaweza pia kuongeza chumvi ya ziada kwenye chakula chako.Tatizo la njia hii ni kuwa, chakula kinahisika kuwa na chumvi zaidi ya radha zingine.

Ukiona viwiko, vidole, miguu, mikono au kope za macho zinavimba (kuvimba kusikotokana na ajali au jeraha), au unaharisha zaidi, usitumie chumvi kwa siku 2 mpaka 3, kunywa maji halisi pekee na kisha siku ya tatu, endelea kuchukuwa chumvi tena, lakini ichukuliwe taratibu. Kamwe usitumie chumvi zaidi ya robo tatu gramu kwa kila nusu lita ya maji.

Kumbuka chumvi ikizidi hupelekea kuharisha.
Dr.Batmanghelidj anasema, kunywa maji matupu kunaweza pelekea mwili kupoteza baadhi ya madini na vitamini zake mhimu nje ya mwili na hivyo kutozipa seli muda wa kutosha kuyatumia maji. Inashauriwa kutumia vidonge vyenye vitamini nyingi kwa pamoja (multivitamins) katika kila mlo wako ili kurudishia kile kitakachokuwa kimepotea (hasa ikiwa haufanyi mazoezi na kula kiasi kingi cha mboga za majani).

Uvimbe utakapokuwa umepotea au umeacha kuharisha, unaweza kuendelea na mpango wako wa kunywa maji nusu ya uzito wako katika aunsi ingawa mara hii utayachukua kwa kiasi kidogo.

Kwa siku nzima, anza kuongeza kiasi cha unywaji wako wa maji mpaka ufikie tena nusu ya uzito wako katika aunsi, anza pia kuchukua chumvi pamoja na maji. Unatakiwa kuhakikisha kuwa unapata gramu 150 za madini ya iodine kwenye “multivitamins” zako kila siku mpaka gramu 450 kwa siku.

Kisha kunywa maji, maji yanapaswa kubaki ndani ya mwili masaa 2 mpaka 2 na nusu ili kuupa mwili muda wa kutosha kuyatumia maji hayo vizuri.

Ikiwa inakulazimu kukojoa (peeing) chini ya muda wa masaa 2 tangu unywe maji, utalazimika kuacha kunywa maji matupu, jaribu kunywa juisi (uliyotengeneza mwenyewe) ya chungwa, ya limau au ya zabibu au juisi nyingine yeyote isipokuwa kwa watu wanaosumbuliwa na pumu (asthma) ambao hawatakiwi kunywa juisi ya chungwa.

Wakati huo huo mhimu kukumbuka kuongeza robo