Dec 22, 2013

Bishop Joe: KUWENI NA HOFU YA MUNGU katika Kuumaliza mwaka huu na kuanza vema mwaka 2014


WANANCHI wametakiwa kuwa na hofu ya Mungu katika kipindi hiki cha kuumaliza na kuuanza mwaka mpya wa 2014 kwa kudumisha amani na utulivu ili kuvuka kwa usalama.

Wito huo umetolewa na Askofu wa makanisa ya Bread of Life, Joe Imakando, wakati akiongea na Highlands FM katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe mkoani Mbeya.

Askofu Imakando ameeleza kuwa watu wanatakiwa kuwa karibu na huduma za kidini ili kuimarisha amani na usalama katika kipindi hiki na kusema kuwa watu wanatakiwa kulinda amani yao wao wenyewe.

Pia amesifia uongozi wa kisiasa na serikali ya nchi ya Tanzania kwa kusema kuwa ni bora kwani wanatatua matatizo yao bila ya kusababisha uvunjifu wa amani.