Nov 15, 2013

Mourad wa Azam: Siamini kuitwa TAIFA STARS


BEKI wa kati wa Azam FC, Said Mourad maarufu kama ‘Mweda’, amesema kuwa hakutarajia kabisa kuitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, baada ya kuumia kifundo cha mguu wakati akiichezea timu ya pili ya taifa.
Mourad ameeleza kuwa ameumia kifundo cha mguu ambacho aligongwa na Sure Boy, Salum Abubakar wa Azam, ambaye pia alichezea Taifa Stars.
Amesema kuwa ilikuwa bahati mbaya kwani alitega mguu vibaya ndipo akaupiga na kuumia kwa sababu viatu vyake vilikuwa vigumu sana.
Ameongeza kuwa anamshukuru sana Mungu kwa kuitwa Taifa Stars na anazidi kumuomba aendelee kufanikiwa katika timu hiyo kwa sababu anaamini kuwa ana uwezo.
Mourad aliumia kipindi cha kwanza katika mechi hiyo na kutoka nje, ambako alifungwa bandeji na barafu kutokana na maumivu makali.