Aug 31, 2012

MSANII CHRIS AJIUA

Mwanzilishi na mmiliki wa Violator Entertainment anayefahamika kwa jina la Chris Lighty ambaye pia alikuwa mwanamuziki wa HipHop amefariki dunia siku ya jana huko Marekani baada ya kujipiga risasi.

Chriss amejiua kutokana na tafrani iliyokuwa ikimsumbua baina yake yeye na mkewe chanzo kikiwa ni upotevu wa fedha na madeni yanayoikabili familia hiyo.

Chris ambaye alikuwa akidaiwa Dola Milioni Tano ($5 m.) na IRS alilazimika kuuza baadhi ya vitu vyake ikiwa pamoja na hotel ili kuweza kulipa deni hilo hali iliyomfanya kuonekana kama amechanganyikiwa na muda mwingi walikuwa hawaelewani na mkewe Veronica.

Chris hatasahaulika kwa kuviinua vipaji ambavyo kwa sasa ndio nguli wa muziki duniani kama vile; 50 Cent, Maria Carey, Busta Rhymes, Diddy, Jarule na wengine KIBAOOO. RIP MAN..