Dec 13, 2013

ELIMU: Dhana potofu kuhusu vyakula na kisukari

Kuwa na elimu sahihi kuhusu maradhi ya kisukari kwa wagonjwa wa kisukari na watu wasio wagonjwa ni njia madhubuti ya kuyakabili maradhi hayo... Makala hii yatabainisha mambo yanayotafsiriwa vibaya baina ya vyakula na maradhi ya kisukari.
Dawa pekee hazidhibiti kisukari..
Baadhi ya watu wanaamini kuwa...
kutumia dawa zaidi bila ya kuwa na nidhamu ya vyakula na kufanya mazoezi kunatosha kudhibiti maradhi ya kisukari. Wasomaji wetu walituambia kuwa walitumia dawa za asili kutibu kisukari, walipopima hospitali kiwango cha kisukari kilikuwa cha kawaida na wao afya zao zilikuwa nzuri.
Wanashangaa baada ya miezi kadhaa ugonjwa wa kisukari ulirudi tena.. Walipoulizwa ratiba yao ya ulaji ilibainika kuwa hawafuati ulaji bora. Kwa mfano, walikiri kuwa wanakula zaidi vyakula mbalimbali na wengine wanakula nyama kila siku.
Pia, wengi wao walikiri kutokufanya kazi za kutoka jasho wala mazoezi ya viungo kutokana na kutingwa na shughuli za kutafuta fedha... Kwa watu hasa wenye aina ya maisha kama hayo, kuamini kuwa dawa pekee zitamaliza au kudhibiti maradhi ya kisukari ni ufahamu potofu.
Lazima upigwe vita kwa nguvu zote ikiwemo elimu... Kwa nini dawa pekee haitoshi?.. Ili mtu awe hai lazima mwili wake uwe na kiwango cha sukari kinachotakiwa kiafya. Kwa hiyo, mtu huyo lazima awe anakula vyakula kila siku. Na hapo ndipo kwenye changamoto ya maradhi ya kisukari. NI KUTOKA MWANANCHI..