Nov 24, 2010

ZAIDI YA WATU 378 WAPOTEZA MAISHA CAMBODIA

WATU wasiopungua 378 wamepoteza maisha  na wengine 755 kujeruhiwa baada ya kukanyagana katika daraja la mto Bassac baada ya hofu kuzuka wakati wa Sherehe za Maji nchini humo. Waziri Mkuu wa nchi hiyo Hun Sen alisema  tukio kama hilo halijawahi kutokea tangu miaka ya 1970 enzi za utawala wa  Khmer Rouge ya mapema jana jumatata kuwa leo yaani Jumanne itakuwa ni siku ya kutambua miili ya marehemu na kuongeza kuwa Juhudi za kuitafuta miili miingine zinaendelea katika mto huo.


Waziri huyo alitangaza kuwa siku ya Alhamis itakuwa siku ya Maombolezo nchini humo na Mamlaka husika zimetakiwa kushusha bendera nusu mlingoti ifikapo siku hiyo na kusema kuwa  Serikali ya nchi hiyo itazilipa familia zilizofikwa na msiba kwa mtu liyekufa itatoa dola 1250 sawa na shilingi milioni 2 za kitanzania  gharama za mazishi na kwa kila aliyejeruhiwa  kiasi cha dola 250 sawa na kiasi cha shilingi laki tatu.
Pole kutoka kwa Abbin Mbungula.